Mtoto wa miaka sita ashinda mashindano ya kuhifadhi Quraan mkoa Arusha, Amana Benki yamwaga Zawadi. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 24 March 2025

Mtoto wa miaka sita ashinda mashindano ya kuhifadhi Quraan mkoa Arusha, Amana Benki yamwaga Zawadi.

 


Sheikh wa mkoa Shaban Juma akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi

Meya wa jiji la Arusha Maximillian Irange akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi




Mratibu wa Jukwaa la vijana wa Kiislam mkoa Arusha Mussa Juma akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi 

Amir jukwaa la vijana Kassim Degega akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi 

Meneja wa Amana Benki Arusha, Ally Mdee akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi 



Mussa Juma,maipac


Maipacarusha@gmail.com


Arusha.Mtoto mwenye umri wa miaka sita amekuwa ni miongoni mwa washindi 9 ya mashindano ya kusoma na  kuhifadhi Quraan Tukufu yaliyoandaliwa jana na Jukwaa la vijana wa Kiislam mkoa Arusha.


Katika Mashindano hayo yaliyoshirikisha vijana 31 katika kuhifadhi na kusoma vyema juzuu tatu,tano na 10 ,mgeni rasmi alikuwa ni Sheikh wa mkoa Arusha,Sheikh Shaban Juma.


Mtoto huyo wa miaka sita, Is'haqa  Yahya Giriba alizawadiwa zawadi kadhaa ikiwepo luninga ya nchi 24  nafasi ya pili alishinda Mohamed  Abdalah ambaye alizawadiwa radio kubwa  huku nafasi ya tatu akishinda  Nasmah Omar ambaye pia alizadiwa radio na zawadi

 nyingine.


Katika mashindano hayo ambayo yalifanyika ukumbi ya Arusha Mall na kujudhuriwa na mamia ya watu,  Sumaiya  Abubakar alishinda katika kusoma na kuhifadhi juzuu tano na kuzawadiwa zawadi kadhaa ikiwepo TV nchi 24.


Mshindi wa pili wa juzuu tano alikuwa Sphia Rajab aliyezawadiwa TV wakati mshindi wa tatu Tamir Idrisa alizawaduwa zawadi kadhaa ma Radio kubwa.


Katika mashindano hayo ambayo mdhamini mkuu alikuwa ni Banki ya Amana,Ibrahim Ayoub alishinda juzuu 10 na kuzawadiwa zawadi kem kem ikiwepo TV nchi 32.


Mshindi wa pili alikuwa ni  Yusra Yasin ambaye alizaeadiwa zawadi kadhaa na TV nchi 24 huku Nuswiba Nashir alishinda nafasi ya tatu na kuzawadiwa TV na zawadi kadhaa.


Sheikh wa mkoa Sheikh Shaban Juma akizungumza katika mashindano hayo ,alipongeza jukwaa la vijana kuandaa mashindano hayo ambayo ni muhimu sana katika kuhamasisha usomaji wa Quraani tukufu.


Sheikh Shaban Juma alisema Mwenyezimungu amehimiza usomaji wa quraani tukufu kwani jambo zuri na linafaa kuendelezwa.


Aliwataka waislam na vijana wa kislam mkoa Arusha,kuendeleza usomaji mzuri wa Quraani kwani kuna manufaa makubwa na thawabu nyingi hasa kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhan.


Sheikh wa mkoa pia aliwataka Waislam mkoa Arusha,kuunga mkono kazi nzuri ambazo zinaendelea kufanywa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Meja wa jiji la Arusha,Maximillian Irange akizungumza katika mashindano hayo ,aliwataka Waislam mkoa Arusha kuendeleza umoja na.mshikamano baina yao


Meya wa Jiji la Arusha pia aliwataka wakazi wa Arusha pia kujitokeza katika kampeni ya upandaji miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.


Meneja wa Amana Banki mkoa Arusha,Ally Mdee alisema lengo la benki hiyo kudhamini mashindano hayo ni kuwaunganisha waumini katika mambo ya kheri.


Mdee hata hivyo aliwataka waislam mkoa Arusha kujitokeza kufungua akaunti katika benki hiyo na kuachana miamala yenye riba na mikopo ya kausha damu .


Alisema Amana benki ina huduma mbalimbali ikiwepo kuweka fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kwenda kuhiji Makka na kwenda Umra.


"Pia tunatoa mikopo kwa misingi ya Sharia hivyo karibuni"alisema


Meneja huyo pia alitangaza zawadi ya kuwafungulia akaunti katika benki hiyo washindi wote wa mashindano hayo na kuwapa zawadi kadhaa.


Amir wa Jukwaa la Waislam mkoa Arusha,Kassim Digega aliwashukuru mamia ya waislam kwa kuhudhuria mashindano hayo na Benki ya Amana kuwa mdhamini mkuu.


Degega alisema mashindano hayo ya kwanza kuandaliwa na jukwaa la vijana wa Kiislam mkoa Arusha yamekwenda vizuri na Allah akipenda mwakani yatakuwa makubwa zaidi .


Katika mashindano hayo jukwaa la vijana lilitoa tende kwa watu wote ambao walishiriki na pia zawadi mbalimbali ikiwepo misahafu na Juzuu.


Mwisho.

No comments: