Na Mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com
Askofu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) Dayosisi ya Arusha, Philemon Mollel amehimiza maridhiano baina ya vyama vya siasa tunapoelekea uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika ibada ya pasaka iliyofanyika katika Parokia ya Arusha, Askofu Mollel amesema ni vyema watanzania wote wakashikammana na kuwa kitu kimoja wakati huu Taifa linapojiandaa Kwa uchaguzi wa Rais, Wabunge na madiwani utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Amewataka viongozi wa serikali kuwa wavumilivu na wenye subira hata pale inapotokea maneno ya kuudhi miongoni mwa wanasiasa wenzao
"Nawasihi viongozi kuacha kuwekana ndani hata katika mambo ambayo yangeweza kumalizwa Kwa majadiliano" Alisisitiza Askofu Mollel.
Aidha Askofu Mollel amewatahadharisha watanzania kujiepusha na ushabiki wa kisiasa ambao unaweza kutuingiza katika machafuko jambo ambalo linaweza kuepukika Kwa njia ya mazungumzo.
Amesema Kwa muda mrefu Tanzania imekua ndio kimbilio Kwa nchi zinazotawaliwa na machafuko Kwa kuonana kuwa ndio sehemu salama ya kukimbilia hivyo tusiichezee Amani tuliyonayo.
Amewasihi viongozi wenzake wa dini Maaskofu, wachungaji, Mashehe, mapadri na viongozi wengine wa kijamii kujiepusha na mtego wa kushabikia upande mmoja miongoni mwa wanasiasa.
"Nawasihi viongozi wenzangu wa dini na watanzania Kwa ujumla wetu, tujielekeze Kwa mwenyezimungu ajaalie uchaguzi wetu wa oktoba mwaka huu uwe wa Huru wa Haki na Amani" alisema
Askofu Monaban ambaye kabla ya kuingia katika Utumishi aliwahi kugombea nafasi kadhaa za kisiasa.
Katika hatua nyingine amewataka waumini wenye uwezo wa kuongoza kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali na wengine wajitokeze wakati wa kampeni kasikiliza na kuchagua viongozi watakaoona wanafaa.
...mwisho.....
No comments:
Post a Comment