TASAC yawatahadharisha Wakala wa Forodha Tanga - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 22 April 2025

TASAC yawatahadharisha Wakala wa Forodha Tanga

 



Na: Burhani Yakub Tanga.


maipacarusha20@gmail.com 



Viongozi wa Taasisi na  kampuni binafsi zinazotoa huduma kupitia usafiri kwa njia ya maji wa Mkoa wa Tanga wametahadharishwa kuwa kama wataendelea kufanya kazi bila kwendana na kasi ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika bandari ya Tanga ipo hatari ya wageni kuchukua nafasi zao.

Mkurugenzi wa Udhibiti wa usafiri kwa njia ya maji katika Shirika la uwakala wa meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali(pichani )ametoa angalizo hilo wakati wa kikao cha wadau wa usafiri kwa njia ya maji wanaofanya shughuli zao katika bandari ya Tanga.

Uwekezaji uliofanywa na Serikali katika bandari ya Tanga ni mkubwa unaohitaji watendaji katika kampuni na Taasisi binafsi pamoja na za Serikali kutoa huduma kwa kasi kubwa.

Amesema uwekezaji katika bandari ya Tanga umesababisha idadi ya meli zinazoitumia kupakua shehena kuongezeka kwa kuvuka makadirio.

"Kampuni za watoa huduma zinazodhibitiwa na TASAC lazima ziache kufanya kazi kwa mazoea,badala yake zitii sheria na taratibu zilizowekwa,zishiriki ulinzi na usalama wa raslimali za nchi,utunzaji wa mazingira ya maji na kutoa huduma kwa kasi inayohutajika na wateja wote Duniani"amesema Mlali.

Mkurugenzi huyo ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili watoa huduma kwa njia ya maji kuwa ni pamoja na mgongano wa maslahil baina ya mawakala wa forodha dhidi ya mawakala wa meli,watoa huduma ndogondogo dhidi ya mawakala wa meli.mawakala wa meli dhidi ya TPA na mawakala wa forodha dhidi ya TPA.

Amesema TASAC ilianzishwa chini ya Sheria namba 14 ya mwaka 2017 na kupewa majukumu mbalimbali likiwamo la udhibiti wa usafiri kwa njia ya maji ambayo hufanyika Kwa kuwasimamia watoa huduma walio katika mnyororo wa usafiri kwa njia ya maji.

Katibu wa Chama Cha Mawakala Tanzania (Tafma) Mkoa wa Tanga, Bakari Juma ameiomba TASAC kuongeza nguvu zake katika Mkoa wa Tanga ili kutoa msukumo zaidi.

"Tunaomba TASAC iongeze msukumo wa utendaji kazi wake Mkoa wa Tanga ili tuweze kuendana na kasi ya uwekezaji uliofanywa Tanga"amesema Bakari.

Hata hivyo baadhi ya mawakala waliozungumza katika kikao hicho wamesema imekuwa ikijitokeA changamoto ya uhaba wa makontena ya kusafirishia bidhaa ambapo kampuni zinazoshughulia zimeahidi kuifanyia kazi.

No comments: