Na: Mwandishi wetu,Maipac
maipacarusha@gmail.com
Siku hizi watu hutumia wakati mwingi kwenye simu zao za rununu. Hata hivyo, huenda hatujui jinsi simu za mkononi zinavyofanya kazi na zinavyoathiri miili yetu.
Katika uchambuzi huu fatilia madhara ya simu yako na jinsi unavyoweza kupunguza madhara hayo.
Je, mionzi katika simu zetu ina madhara kiasi gani? Je, matumizi ya simu mara kwa mara husababisha saratani? Na unaweza kujilindaje?
Wanasayansi wamekuwa wakitafuta majibu ya maswali haya kwa miaka mingi. Lakini hakuna utafiti ambao umechapishwa hadi sasa kujibu maswali hayo kwa uwazi. Kwa hiyo, mjadala kuhusu suala hili unaendelea.
Tunajua kwamba mawasiliano ya simu huzalisha mawimbi ya sumakuumeme kupitia masafa ya redio. Mawimbi haya ni dhaifu sana kuliko mionzi ya ionizing kama vile ya X-rays. Mionzi ya ionizing hupenya kwenye tishu za mwili wa binadamu, kuharibu seli na kubadilisha muundo wa DNA.
Katika maisha yetu ya kila siku mawimbi ya redio yanapita; kutoka vituo vya redio hadi mionzi kutoka microwave. Inajulikana kuwa mionzi isiyo ya ionizing haina nishati ya kuharibu muundo wa DNA.
Hata hivyo, kulingana na taarifa kwenye tovuti ya Shirika la Saratani la Marekani (ACS), simu za mkononi huongeza hatari ya kupata uvimbe kwenye shingo na kichwa, na pia kwenye ubongo. Watafiti wa ACS wanashauri kutumia simu za rununu kwa muda mdogo kadiri iwezekanavyo.
Nguvu kubwa ya mawimbi ya redio hupasha joto tishu za mwili. Hii ni kanuni sawa na ambayo hutumika katika microwave ili ifanye kazi. Ingawa kiwango cha nishati ya mionzi inayotolewa kutoka na simu za mkononi ni ya chini sana na haiwezi kuongeza joto la mwili wa binadamu
Ni simu gani hutoa mionzi mingi?
Ili kupima hatari za kiafya zinazoweza kutokea, wanasayansi wamebuni kipimo cha SAR. Hiki kinaonyesha ni mionzi kiasi gani inafyonzwa na tishu za mwili wa mwanadamu wakati wa kutumia simu ya rununu.
Takwimu zinatofautiana kulingana na aina ya simu, na watengenezaji wanahitajika kutangaza kiwango cha mionzi katika simu. Taarifa hiyo hupatikana mtandaoni au katika mwongozo wa mtumiaji wa simu. Lakini watumiaji wa simu hawajali sana hii.
Ofisi ya Shirikisho ya Kinga dhidi ya Mionzi (BfS) imeunda hifadhidata maalum ili kulinganisha simu za zamani na mpya zilizo na viwango vya juu vya mionzi.
Kwa bahati mbaya, hakuna ushauri wa kina juu ya kiwango salama cha mionzi ya simu ya mkononi. Kwa mfano, nchini Ujerumani kuna chombo cha serikali kinachoitwa Der Blaue Engel, ambacho kinaweka viwango kwa upande wa mazingira. Taasisi hii inachukulia simu za rununu kuwa salama, ikiwa ufyonzaji wa mionzi hauzidi wati 0.60.
Simu zote kwenye orodha ya hapo juu zinazidi kiwango hiki mara mbili. OnePlus 5T, ambayo inaongoza katika orodha, ina kiwango cha 1.68 watts / kg.
Ili kujua kiwango cha mionzi katika simu yako, angalia mwongozo wake au tembelea tovuti ya mtengenezaji wa simu au tovuti ya Tume ya Shirikisho ya Mawasiliano ya Marekani.
Nini kifanyike ili kujilinda??
.Antena inayopitisha mawimbi ya redio iko ndani ya simu yako kwa sasa. Mawimbi yanapoteza nguvu yanapokuwa mbali na simu. Watumiaji wengi hushikilia simu masikioni mwao wakati wa kuzungumza. Kadiri antena inavyokaribia sikio, ndivyo mionzi inavyokuwa karibu nawe.
Kwa hiyo, unapaswa kupunguza muda unaotumia simu yako. Au tumia simu yako na kipaza sauti (loud speaker) au tumia vipokea sauti vya masikioni (ear phone), na hivyo utakuwa umeshiklilia simu mbali na kichwa chako.
Jaribu kutumia simu yako mahali penye mawimbi mazuri ya mnara. Kadiri mnara unavyopungua, ndivyo simu yako inavyotumia nguvu zaidi. Na ni bora kununua simu zenye mionzi ya chini.
No comments:
Post a Comment