KOKA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MAENDELEO YA WANAKIBAHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 27 April 2025

KOKA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MAENDELEO YA WANAKIBAHA





 Na Julieth Mkireri, MAIPAC KIBAHA


maipacarusha20@gmail.com 


MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Sylvestry Koka amesema maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano yametokana na uongozi  mzuri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Serikali ya awamu ya sita.


Koka ameyasema hayo April 27 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM)  2020-2025 kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa Jimbo.


Amesema kitendo cha kuwa na Rais msikivu kimekuwa chachu ya maendeleo katika Jimbo la Kibaha mjini ambapo kero katika sekta mbalimbali zimetatuliwa na hivyo kuwafanya wabunge kumsaidia kwa urahisi utekelezaji wa ilani ya Chama.


"Raisi wetu ni mama msikivu anapoelezwa shida za wananchi hachelewi tutoa maelekezo ya utatuzi wa haraka kwa maendeleo yaliyopatikana kwenye Jimbo letu tuna kila sababu ya kumpa kura za heshima muda utakapofika," amesema.


Mwenyekiti wa chama hicho Kibaha mjini Mwajuma Nyamka amesema chama hicho kinasimamia utekelezaji wa ilani ambapo miradi mbalimbali umetekelezwa  kwa fedha kutoka Serikali kuu na mapato ya ndani.


Awali Katibu wa CCM Kibaha mjini Isack Kaleiya alisema wanaendelea kusimamia taratibu na kanuni za chama na kwa kila anayeenda kinyume na kanuni na taratibu za chama hatua zinachukuluwa kupitia kamati ya maadili.


Wajumbe zaidi ya 8000  wa CCM kutoka kata 14 wa ameshiiriki mikutano ya Jimbo iliyofanyika kwa siku tano kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani iliyowasilishwa na Mbunge huyo.


Mwisho 


No comments: