LION'S CLUB WAKABIDHI VIFAA TIBA JIMBO LA KOJANI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 22 April 2025

LION'S CLUB WAKABIDHI VIFAA TIBA JIMBO LA KOJANI

 



Na Julieth Mkireri , MAIPAC 


maipacarusha20@gmail.com 


TAASISI ya Lions Club imekabidhi vifaa tiba kwa Mbunge wa Jimbo la Kojani Pemba Hamad Chande kwa ajili ya vituo vya huduma za afya jimboni humo.


Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika April 21 jijini hapa Mwenyekiti mstaafu wa Taasisi ya Lions Club Muntazir Bharwani amesema walipokea maombi kutoka kwa Waziri huyo kuhusiana na uhitaji  wa vifaa tiba ambavyo kupitia michango yao wameweza kununua na kuvikavidhi.


Bharwani amesema wataendelea kutoa ushirikiano kusaidia jamii katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo mbali ya kukabidhi vifaa tiba hivyo pia watachimba kisima cha maji katika kituo cha afya Minungwi.


Mbali ya kukabidhi vifaa hivyo Lions Club imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ya vyakula kipindi cha mwezi wa Ramadhani kwenye maeneo tofauti ikiwemo mkoa wa Pwani na Dar es Salam, pamoja na huduma ya matibabu ya macho gharama ambazo zinatokana na michango ya wanachama na wadau wa maendeleo.


Hamad Chande ambaye pia ni Naibu Waziri wa fedha ameishukuru Taasisi hiyo huku akizitaka Taasisi nyingine kufanya mambo ya kijamii kama ilivyo Lions Club.


"Kutokana na umuhimu wa Taasisi kama Lions Club hapa nchini na wengine tuunganishe nguvu twende tukawahudumie wananchi tuunge mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita kwa vitu ambavyo imevifanya ikiwemo ujenzi wa vituo vya huduma ya afya.


Katika Hafla hiyo ya makabidhiano Naibu Waziri Chande amejiunga na Taasisi hiyo kushirikiana kusaidia jamii kwa vitu mbalimbali huku akiomba kufunguliwa kwa ofisi Visiwani Zanzibar kama ilivyo kwa mkoa wa Dar es Salam.


Naye Asimuna Kipingu ambaye amejiunga na Taasisi hiyo katika hafla hiyo amepongeza kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo kwa kuungana na Serikali kuifikia Jamii.


Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na viti mwendo kwa ajili watu wenye Ulemavu, magongo ya kutembelea na Mashine za kupima presha.


Mwisho.

No comments: