THRDC, serikali wajadili uwepo wa Sera ya watetezi wa haki za binaadamu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 23 April 2025

THRDC, serikali wajadili uwepo wa Sera ya watetezi wa haki za binaadamu

 





Na: Mussa Juma,maipac


maipacarusha@gmail.com


 Kilio cha muda mrefu cha watetezi wa haki za binaadamu nchini kuwa na sera ya kuwatambua na kuwalinda kimeanza kusikika baada ya mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wizara (Katiba na Sheria) na CHRAGG kufanya kikao kazi kilicholenga  kuandaa sera ya watetezi wa haki za binadamu nchini.


Kikao hicho pia kulilenga kuweka  mazingira salama kwa watetezi  wanaotetea na kulinda haki za binadamu nchini.


Katika taarifa ya THRDC kwa vyombo vya habari imeeleza Kikao hicho kiliwashirikisha na Afisa Programu kutoka Kitengo cha Kimataifa cha Huduma za Haki za Binadamu (ISHR)-Geneva, na Mshauri Mstaafu UN juu ya masuala ya uhuru na kujumuika ndugu Clemency Voule, Mratibu Taifa THRDC, wakili Onesmo Ole Ngurumwa na serikali ni wataalamu wa sera wakiongozwa na Mbaraka  Stambuli, Mkurugenzi wa Sera na Mipango pamoja na Katibu Mkuu Wizara, Eliakim Maswi aliyehitimisha kikao hiki. 


Wizara imepokea rasmi mapendekezo hayo na kupongeza THRDC kwa ushirikiano wake unaotumia taaluma ya sheria na ujuzi katika kukuza hali ya haki za binadamu nchini Tanzania. 


Wizara imeiweka sera hii katika rejea muhimu na kuahidi kuitumia kikamilifu kwa masilahi mapana ya kitaifa ikiwa  ni pamoja na hatua kadhaa ambazo Wizara imeushauri Mtandao kuendelea kupitia ili kufikia lengo hili Muhimu. 



Wizara imeshauri kuhusisha masuala ya Watetezi wa haki za binadamu katika sera mbalimbali na mikakati inayoendelea kuandaliwa kwa sasa ikiwemo sera ya mfumo wa haki jinai na mpango kazi wa haki za binadamu na biashara.


Wizara pia, imependekeza kufanya marekebisho ya sheria zilizopo ili kushughulikia mapungufu ya sasa kama  hatua ya awali katika kuwatambua na kuwapa ulinzi watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. 


Kutokana na kikao hicho, MoCLA na THRDC wamekubaliana kufanya ziara ya mafunzo katika nchi ambazo tayari zimepitisha sera au sheria hii na kupata uzoefu kwa ajili ya kuimarisha mchakato wa sera ya ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,  alisisitiza utayari wa Serikali kushiriki katika mchakato wa pamoja, jumuishi na unaozingatia maslahi ya Taifa katika kuimarisha ulinzi kwa watetezi wa haki za binadamu na Haki za Binadamu kwa ujumla. 


Mwisho

No comments: