![]() |
| Picha ya pamoja ya washiriki wa semina hiyo maa baada ya kumaliza mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika katika ukumbi wa nikutano Golden Rose Hotel jijini Arusha |
![]() |
| Mratibu na msimamizi wa miradi toka UNDP ndugu Faustine Ninga akiwaundisha wakurugenzi na maafaisa mipango hao mambo ya kuzingatia wakati wa utekelezaji wa miradi yaoiliyofadhiliwa na UNDP. |
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella |
![]() |
| Mratibu na msimamizi wa miradi toka UNDP ndugu Faustine Ninga kushoto akiwa na Afisa miradi wa MAIPAC ndugu Andrea Ngobole baada ya kujengewa uwezo wa namna ya kusimamia miradi inayodhaminiwa na UNDP |
![]() |
| Mratibu na msimamizi wa miradi toka UNDP ndugu Faustine Ninga akiwafundisha wakurugenzi na maafaisa mipango hao mambo ya kuzingatia wakati wa utekelezaji wa miradi yaoiliyofadhiliwa na UNDP. |
Mkuu wa mkoa Arusha, John Mongella, amewataka watendaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)mkoa wa Arusha, kufanyakazi kwa kuzingatia sheria ili kuchochea maendeleo katika jamii badala ya kuchochea migogoro.
Akizungumza katika mkutano wa kuwajengea uwezo watendaji wa mashirika 15 yanayofanya miradi kwenye jamii za pembezoni, ambayo inafadhiliwa na shirika la misaada la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP), Mongella alisema mashirika yasiyo ya kiserikali yanawajibu kusaidia kuchochea maendeleo na kukabiliana na umasikini katika jamii.
Mongella alisema Serikali mkoa wa Arusha, itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanyakazi nzuri kwa kuzingatia sheria, taratibu miongozo ambayo imepitishwa.
Mkuu huyo alipongeza shirika la UNDP kupitia shirika la MUMUTIE Woman Organization(MWO) kwa kusaidia mashirika madogo mkoa wa Arusha,katika kuyajengea uwezo juu ya usimamizi wa miradi, uongozi bora kuandika ripoti na usimamzi wa fedha.
Awali Mkurugenzi wa MW0, Rose Njilo alisema lengo la uzinduzi huo pia ni kutoa taarifa kwa umma, juu ya miradi ambayo itakwenda kutekelezwa katika maeneo kadhaa nchini na mashirika 15.
"tumewaita hapa wakurugenzi na waratibu wa miradi katika mashirika 15 ambayo yamepatiwa fedha na tunatarajia kuwajengea uwezo ili waweze kuendesha vyema miradi yao"alisema.
Maria Yona mkazi wa eneo la Eyasi wilayani Karatu,alisema wanatarajia kunufaika na miradi ambayo itatekelezwa katika maeneo yao, katika kuwajengea uwezo kuhusiana na masuala ya mazingira,mabadiliko ya tabia nchi na umasikini.
"sisi kwa jamii yetu ya wahadzabe tunaimani tutanufaika na miradi hii ya UNDP katika maeneo yetu kwani bado tupo nyuma na tunakabiliwa na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi"alisema.
Awali mratibu wa miradi midogo ya UNDP ya kuhusiana na masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi,Faustine Ninga aliwataka watendaji wa mashirika ambayo yamepata ruzuku kufanya kazi kwa kuzingatia mikataba .
Alitaka watendaji na maafisa miradi kushirikiana na jamii katika utekelezaji wa miradi,kuwa waadilifu katika matumizi ya fedha na kuandika ripoti kwa wakati.






No comments:
Post a Comment