CHEKI HAPA MASHINDANO YA GOLF ARUSHA OPEN 2022 YALIVYOFANA, watoto waweka historia - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 15 August 2022

CHEKI HAPA MASHINDANO YA GOLF ARUSHA OPEN 2022 YALIVYOFANA, watoto waweka historia

Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo akimkabidhi zawadi mshindi wa jumla wa mashindano ya Golf Jay Nathwani wa klabu ya Gymkhana Arusha

 

Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo akimkabidhi zawadi mshindi wa jumla wa mashindano ya Golf Jay Nathwani wa klabu ya Gymkhana Arusha
Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo akimkabidhi zawadi mshindi wa jumla wa mashindano ya Golf Jay Nathwani wa klabu ya Gymkhana Arusha

Mchezaji wa Golf Jay Nathwani wa klabu ya Gymkhana Arusha, juzi ametwaa kikombe cha  mashindano ya Golf ya Arusha open 2022, ambayo yalishirikisha wachezaji 117 kutoka nchi za Afrika ya Mashariki.


Nathwani alishinda kwa kupata jumla ya point 154 na nafasi ya pili ilichukuliwa na aliyekuwa bingwa mtetezi wa mashindano hayo Victor Joseph wa kutoka klabu ya Gmykhana ya jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya bima ya Reliance,mshindi kwa upande wa wasichana alikuwa ni  Neema Ulomi akifatiwa na Stella Emmanuel.

Kwa upande wa watoto  mshindi alikuwa ni Mohamedasad Meloncelli huku katika daraja la A, mshindi alikuwa ni Aliabbas Kermali akifatiwa na Nathaniel Itinda, huku Raju Ladhia akishinda upande wa daraja B akifatiwa na Dismas Seth na daraja C alishinda Dian Vaja akifatiwa na Tinka Sour.

Akizungumza katika hafla ya kutoa zawadi,Mtendaji mkuu kampuni ya ya bima ya Reliance  Ravi Shankar  aliahidi kampuni hiyo kuendelea kudhamini mashindano hayo kila mwaka ili kukuza mchezo wa golf nchini.

Shankar alisema kampuni hiyo imefarijika kuona idadi ya washiriki hasa wanawake na vijana inaongezeka kutoka mwaka jana ambapo washiriki walikuwa 104 tu.

Mkuu wa idara ya masoko ya kampuni ya bima ya Reliance, Joyce Bendera alisema mwaka huu idadi ya wanawake imeongezeka na kufikia 13 na watoto 24.

"tunapenda kutoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapa fursa watoto wao kujitokeza kucheza mchezo huu na Golf kwani ni mzuri"alisema

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi aliyekuwa mgeni rasmi, Mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Mrisho Gambo aliwapongeza washiriki wote katika mashindano hayo kwani pia yanachangia kukuza utalii katika jiji la Arusha.

"tunapongeza kampuni ya bima kuendelea kudhamini kwa mwaka wanne sasa mashindano haya ambayo yanakutanisha wachezaji kutoka Afrika ya Mashariki na kwa Arusha ni fursa ya kukuza Utalii na biashara"alisema.

Menejakampuni ya ya bima ya Reliance  mkoani Arusha Urassa kulia akitoa zawadi kwa mshindi kundi la watoto

 Mtendaji mkuu kampuni ya ya bima ya Reliance  Ravi Shankar  kulia kitoa zawadi kwa mshindi upande wa watoto walioshiriki mashindano hayo
michezo ikiendelea uwanjani

No comments: