![]() |
| Picha ya pamoja ya viongozi wa mila, serikali na wa kamouni ya EACOP mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano |
![]() |
Mshauri elekezi wa mradi huo, katika masuala ya haki za binaadamu, Dk Elifuraha Laltaika Kushoto, katikati ni Laigwanani Joseph Laizer na kulia ni Wendy Brown mkurugenzi wa EACOP wakisaini makubaliano hayo |
NA: MAIPAC TEAM, Arusha
Viongozi wa mila wa Masai,Barbeig,Akie na wataturu wamesaini makubaliano ya kukubali kushiriki katika mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania.
Viongozi hao wamesaini makubaliano na Kampuni ya ujenzi wa bomba la mafuta ya EACOP Tanzania katika hafla iliyofanyika MountMeru hoteli jiini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanyakazi na jamii hizo.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wa mila ,Laigwanani Joseph Laizer amesema wamekubali kuwa na makubaliano na kampuno ya EACOP baada ya kuwashirikisha katika mradi huo.
"sisi kama viongozi tumeridhishwa na makubaliano ya leo na tutakwenda kuwa mabalozi kwa wengine"amesema
Hata hivyo kiongozi huyo ameitaka kampuni ya EACOP kutekeleza yote walioyokubaliana.
![]() |
| Umakini wakati wa utiaji saini ukiendelea |
Mkurugenzi wa kampuni ya EACOP Tanzania, Wendy Brown amesema watatekeleza yote waliyoahidi.
"tutashirikiana katika mpango kazi wa mradi wa bomba la mafuta na tutahakikisha mnanufaika"amesema
Amesema watawashirikisha katika utekelezaji wa mradi, kuzijengea uwezo jamii hizo katika masuala ya kiuchumi, kuzisaidia kupata huduma muhimu kama elimu na afya, kuendeleza masuala tamaduni.
Afisa Nishati kutoka wizara ya Nishati, Yovin Uisso amesema serikali itahakikisha makubaliano yaliyofikiwa baina ya EACOP na jamii hizo yatatekelezwa na pande zote.
Amesema katika kuhakikisha jamii hizo zinanufaika na mradi huo serikali itatoa fursa ya upendeleo kwa baadhi ya vitu ikiwepo ajira.
Mshauri elekezi wa mradi huo, katika masuala ya haki za binaadamu, Dk Elifuraha Laltaika, amesema kampuni EACOP imesaini makubaliano na jamii hizo ikiwa ni kuheshimu sheria na vigezo vya kimataifa zinazolinda haki za jamii za pembezoni.
Amesema masuala ya haki za jamii hizo yamezingatiwa katika mradi huo.
Viongozi waliosaini makubaliano hayo ni kutoka wilaya za Simanjiro, Kiteto, Kilindi, Handeni, Igunga, Kondoa na Hanang.



No comments:
Post a Comment