MAIPAC TEAM, MONDULI
Wananchi wa Kata ya Selela na Engaruka wilayani Monduli mkoa Arusha, wameomba serikali kuwasaidia kuweka uzio katika vyanzo vya maji vya asili katika maeneo yao ili visiendelee kuharibiwa na wanyamapori.
Kata hizo zina vyanzo vya maji vya asili ambazo zimekuwa zikitoa maji kwa mwaka mzima ambayo ndio tegemeo kwa mahitaji ya Maji katika Kata hizo kwa matumizi ya majumbani, kilimo na mifugo
Wakizungumza na waandishi wa habari za Mazingira, kupitia mradi wa Utunzwaji Mazingira kwa maarifa asilia unaoendeshwa na taasisi ya wanahabari ya MAIPAC na taasisi ya CILAO mradi ,unaofadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia program ya miradi midogo na kuratibiwa na taasisi ya jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) walisema kama vyanzo hivi havitawekwa uzio vitaharibika.
![]() |
| Mmama mashuhuri wa kijiji cha selela Halima Mollel upande wa kushoto akieleza vyanzo vya maji vinavyo wanufaisha wakina Mama wa kijiji hicho |
Halima Mollel alisema wanyamapori hasa Tembo wamekuwa wakivamia vyanzo hivyo na kuleta madhara jambo ambalo linaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuwekewa uzio.
“Sisi kama jamii tunavitunza vyanzo hivi kwa maarifa yetu ya asili Sasa tunaomba na serikali kutuunga mkono”alisema
Awali Afisa Misitu wa tarafa ya Makuyuni na Manyara, Happiness Masaki alisema Wananchi wa Selela na Engaruka wametunza vyanzo ya Maji kwa maarifa ya asili na Sasa wananufaika.
![]() |
| Afisa misitu wa Tarafa ya Makuyuni na Manyara, Happiness Masaki akiwaelezea wanahabari vynzo vya maji katika kijiji cha Selela wilayani Monduli |
Masaki alisema Kata hizo kwa Sasa Zina maji mwaka mzima licha ya maeneo mengine kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi.
“Sisi kama serikali tunawapongeza Hawa Wananchi kwa kutumza hivi vyanzo kutokana na kujiwekea sheria ndogondogo za kimila ambazo zimekuwa rafiki kwa vyanzo vya maji na Mazingira”alisema
Katibu wa Kamati ya Mazingira Kata ya Selala,Isack Diagwa alisema Siri ya mafanikio ni kushirikisha jamii katika.utunzwaji vyanzo vya maji.
![]() |
| kiongozi wa kimila Laigwanani upande wa kushoto akielezea namna wazee walivyotumia faini za mifugo kwa yoyote aliyehusika na uharibifu wa vyanzo vya maji na misitu |
“Lichaya ya kuwa na sheria za serikali kutunza maji pia tunatumia maarifa ya asili ambapo kila mwananchi anawajibika kutunza vyanzo hivi ikiwepo kutoingiza mifugo kwenye vyanzo,kutokana mti ama kulima”alisema.

Mradi wa uhifadhi Mazingira kwa maarifa asilia unatekelezwa na taasisi ya wanahabari ya Usaidizi wa jamii za Pembezoni (MAIPAC) na shirika la msaada ya kisheria la CILAO na kuratibiwa na jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF)



No comments:
Post a Comment