WASICHANA WA KIMASAI WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA WAJENGEWA DARASA LA MEMKWA WILAYANI LONGIDO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 26 September 2022

WASICHANA WA KIMASAI WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA WAJENGEWA DARASA LA MEMKWA WILAYANI LONGIDO

Muonekano wa darasa hilo


Mfadhili wa darasa hilo la Memkwa Adrian Scott kutoka shirika la Douglas Scott Foundation akiwa katika picha ya pamaoja na uongozi wa halmashauri na shule hiyo mbele ya darasa

Baadhi ya wanakijiji waliohudhuria makabidhiano hayo wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa

Baadhi ya wanakijiji waliohudhuria makabidhiano hayo wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa

Baadhi ya wanakijiji waliohudhuria makabidhiano hayo wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali



Diwani wa kata ya Engarenaibor Simon Ngonoy akiwashukuru wadahamini kwa ujenzi wa darasa hilo na wanakjiji kwa kujitolea kujenga darasa hilo 

Adrian Scott mfadhili wa darasa hilo na Lilian Lalkaita mkurugenzi wa CORDS wakifurahia zawadi toka kwa kamati ya shule

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Longido Simon Oiteson Laizer wa pili kushoto, mfadhili wa darasa hilo Adrian Scott wa shirika la Douglas foundation pamoja na mkurugenzi wa shirika la Cords Lilian Lalkaita wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kata ya Engarenaibor




Mfadhili wa darasa hilo la Memkwa Adrian Scott kutoka shirika la Douglas Scott Foundation akiwasili shuleni hapo sambamba na Mkurugenzi wa Shirika la CORDS Lilian Lalkaita 


NA: ANDREA NGOBOLE, MAIPAC

 Vijana wa jamii ya Kimasai wa kike na kiume, ambao wamekosa fursa ya kusoma katika mfumo rasmi shule ya Msingi  wamejengewa Darasa ili waweze kusoma na hivyo kujikwamua na ujinga na umasikini.

Darasa hilo limegharimu kiasi cha sh 33.5 milioni, lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 45 na litakuwa katika shule ya msingi Ngoswak iliyopo kata ya Engareinabor wilaya ya Longido mkoani Arusha na limejengwa  na shirika lisilo la kiserikali CORDs.


Akizungumza wakati wa kukabidhiwa darasa hilo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Longido,  Simon Oiteson Laizer alishukuru shirika la CORDs na wafadhili shirika la Douglas Scott Foundation la nchini Australia  kupitia mradi wa  action on poverty kwa  kujenga darasa hilo.

"Darasa hili litasaidia sana vijana ambao hawakusoma katika mfumo rasmi wake hapa kusoma na hivi kupambana na ujinga na umasikini"alisema 

wakifurahia darasa hilo

Mkurugenzi wa shirika la Cords Lilian Lalkaita alisema  darasa hilo litakuwa fursa ya pekee kuwasaidia watoto husuani wa kike ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na shule kwa wakati.

Alisema kuwa mazingira ya jamii za pembezoni hususani wafugaji wa kimasai zinazokabiliwa na changamoto nyingi ambazo hupelekea watoto kutopata nafasi ya kuanza masomo kutokana na kukosekana madarasa maalum ya Memkwa ambayo huwapelekea kutokuwa na ari ya kuanza kusoma masomo hayo ya elimu ya msingi.

Amesema mwaka 2019 na 2020 walikuwa na mradi wa kuandikisha wanafunzi wa Memkwa wapatao 20 na kuanza kufundishwa shuleni hapo lakini kutokana na kukosa chumba maakum cha kuwafundishia walipelekwa shule ya msingi.

Mkurugenzi wa shirika la Douglas Scott Foundation Ndugu Adrian Scott toka Australia amesema wao wanafurahia kusaidia jamii kupata mazingira bora ya kujifunzia kwani elimu ndiyo njia pekee ya kujikomboa toka katika umaskini.

 Naye mkuu wa shule hiyo Kwamboka Nyanami Phirace amewashukuru Cords kwa kuwajengea darasa hilo na kuahidi kushirikiana na uongozi wa kijiji kuhamasisha wazazi kuandikisha wanafunzi wa kutosha darasa hilo na wataanza masomo yao rasmi January 2023.

Aidha ametaja changamoto zinazokabili shule hiyo ni pamoja na kutokuwa na chakula cha mchana kwa wanafunzi na walimu, choo cha walimu, choo cha wanafunzi, upungufu wa vyumba vya madarasa nane, nyumba za walimu na pia ofisi ya mwalimu wa darasa la Memkwa.  

Baadhi ya wanakijiji wakifurahia darasa hilo la Memkwa

No comments: