![]() |
| Ng'ombe wakiwa wamekufa baada ya kula majani |
![]() |
| Majani haya yenye sumu yameota katika maeneo mbalimbali wilaya ya Monduli kutokana na mvua ambazo zimeanza kunyesha hivi karibuni |
NA: MAIPAC TEAM
Majani yenye sumu yameua Ng'ombe zaidi ya 15 katika kijiji cha Losirwa wilayani Monduli mkoa wa Arusha.
Mifugo hiyo, imekula majani ambayo yameota katika maeneo mbali mbali katika kijiji hicho cha Losirwa na Kata ya Selela wilaya ya Monduli.
Mkuu wa wilaya ya Monduli, Fank Mwaisumbe amesema hadi juzi zaidi ya Ng'ombe 15 walikuwa wamekufa kwa kula majani hayo.
Amesema Majani hayo, yameota kutokana na mvua ambazo zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali wilayani Monduli na kawaida huwa ni sumu.
"Nimepata taarifa za mifugo kufa kutokana na majani hayo na sasa tumeagiza ifukiwe ili watu wasile m izoga yake kwani ni sumu"amesema
Amesema zoezi la kufukiwa mifugo ambayo imekufa linasimamiwa na polisi ili kuhakikisha hakuna watu ambao watakula.
Mmoja wa wafugaji ambao mifugo yao imekufa, Lememo Mollel amesema Ng'ombe wamekufa kutokana na kula majani ambayo yameota kutokana na mvua za kwanza.
"hii sio mara ya kwanza, mifugo kufa kila baada ya ukame kutokea mvua zikianza kunyesha majani yenye sumu huota na mifugo wakila hayo majani wanakufa"amesema
Hata hivyo, aliomba Serikali kusaidia upatikanaji wa malisho ya mifugo hasa kipindi hiki cha Ukame.
Daktari wa Mifugo kutoka shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa(FAO) Moses Ole-Neselle amesema kufa mifugo kunatokana na kula majani mabichi ambayo yanasumu kutokana na kutokamaa.
"Mifugo inakufa pia kwa sababu bado utumbo haujazoea kula majani mabishi ambayo hayajakomaa baada ya kiangazi kwanza huwa wanaharisha na wengine kufa kabisa"amesema



No comments:
Post a Comment