SHIRIKA LA CORDS WATOA MSAADA WA TANI 12 ZA CHAKULA KWA KAYA ZENYE NJAA WILAYANI MONDULI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 5 December 2022

SHIRIKA LA CORDS WATOA MSAADA WA TANI 12 ZA CHAKULA KWA KAYA ZENYE NJAA WILAYANI MONDULI

Pichani ni wakazi wa Monduli wakisubiri kugaiwa MSAADA WA chakula Toka SHIRIKA LA cords 


 

Ugawaji wa chakula ukiendelea kwa wakazi hao




NA: mwandishi wetu,Monduli

  Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa Jamii( CORDs ) limetoa msaada wa tani 12 za mahindi ya bure kwa kaya 553 za wilaya ya Monduli mkoa Arusha, ili kukabiliana na njaa .

msaada huo umetolewa kutokana na wakazi wengi wa Monduli kukabiliwa na njaa.

Afisa Miradi wa   CORDs Martha Katua  amesema shirika hilo limetoa msaada huo baada ya kubaini Kaya nyingi kukabiliwa na uhaba wa chakula

Katau amesema wamegawa Tani 12 za Mahindi kwa kaya 553 katika Kata ya Mfereji Wilaya ya Monduli.

Amesema  vijiji ambavyo vimenufaika na msaada huo ni Kijiji Indonyonaado ambacho kimepatiwa Tani 6.5 kwa kugawanywa kwa Kaya 301 na Kijiji cha  Emuruwa jumla ya Kaya 252  zimepata Tani 5.5 za Mahindi.

Mmama akiwa anafunga Debe lake la mahindi alilogaiwa na cords



Mwenyekiti wa Bodi ya CORDs Yohana Ordorop alisema jamii ya wafugaji Monduli inakabiliwa na njaa kutokana na ukame.

"wafugaji wanategemea kuuza mifugo ili wanunuwe chakula ila sasa ukame umeua mifugo na mingine kukonda"alisema




Kaimu Afisa Kilimo , wilaya ya Monduli Theobald Ngobya amesema wilaya hiyo inahitaji tani 28,000  za chakula.

Ngobya alisema kumekuwepo na uzalishaji mdogo wa chakula kwa misimu zaidi ya miwili mfululizo katika wilaya hiyo hatua ambayo imesababisha upungufu wa chakula.

Amesema wilaya hiyo inaupungufu wa mahindi Tani 22,550 na maharage Tani 7578 ili kupunguza tatizo la uhaba wa chakula katika maeneo mengi.

Jeremiah John ameipongeza CORDS kuwapa msaada wa chakula kwani wanauhaba wa chakula.

John ameomba mashirika mengine  na serikali kuwasaidia wanajamii hao.

No comments: