![]() |
| Mhifadhi Mkuu katika hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Neema Mollel akizungumza na wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo |
Mwandishi wetu ,Monduli
Waandishi wa habari nchini, wametakiwa kutumia vyombo vyao vya habari kutangaza vivutio vya Utalii, katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, ambavyo havipatikani katika hifadhi nyingine yoyote nchini, ikiwepo Simba wanaokaa juu ya Miti na uwepo wa chem chem ya maji moto ili kuchangia kukuza uchumi wa Nchi.
Katika hifadhi hiyo ya Taifa ya Ziwa Manyara,pia kuna utalii mpya wa kupita juu ya madaraja ya kamba na kuona chini wanyama wa aina mbali mbali kwa ukaribu zaidi.
Mhifadhi Mkuu katika hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Neema Mollel akizungumza wa wa wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo na baadaye kufanya mkutano mkuu maalum katika kumbi za hifadhi hiyo, alisema bado vivutio vya utalii katika hifadhi hiyo havijulikani
"tumeshukuru leo mmekuja kutembelea hifadhi yetu, ambayo ina mambo mengi mazuri na kama mlivyoona ikiwepo mandhara nzuri baada ya ziwa Manyara kumejaa maji"alisema
Mhifadhi Neema alisema maeneo ya hifadhi ni urithi ambao watanzania wamepewa bure na Mungu hivyo ni wakati muafaka kwa watanzania kutumia likizo ya mwaka kutembelea hifadhi hizo na kupata mapumziko sahihi.
![]() |
| Waandishi wa Habari wakiwa katika picha ya pamoja na mhifadhi Mkuu wa ziwa manayara. |
Alisema hifadhi ya ziwa Manyara ni miongoni mwa hifadhi zenye vivutio vingi ambavyo watanzania wanapaswa kuviona badala ya kuachia wageni pekee waweze kutembelea na gharama yake ni ndogo mtanzania sh 11 800, mtoto shilingi 2200 na magari madogo sh 23,000.
" Hifadhi ya Manyara ni moja ya hifadhi rahisi sana kufikika, ukiwa Arusha mjini ni kilometa chache sana unaweza kutumia hadi kufika katika hifadhi yetu na gharama zetu ni ndogo sana,"alisema
Akizungumzia mkutano mkuu maalum wa chama cha waandishi wa habari mkoa Arusha(APC) uliofanyika katika kumbi zilizopo katika hifadhi hiyo, aliwataka wanahabari kufanya mabadiliko mazuri ya Katiba yao ili kuendeleza chama hicho.
Awali akimkaribisha mhifadhi wa Manyara, Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu alisema waandishi wa habari ni miongoni mwa wadau wakubwa wanaopaswa kutembelea hifadhi za Taifa na kuzitangaza.
![]() |
| Baadhi ya waandishi wakifurahia mandhari nzuri hifadhini ziwa Manyara |
Alisema Waandishi wa habari ni miongoni mwa waandishi ambao wamekuwa wakitoa kipaumbele kutangaza hifadhi za Taifa na kwamba mbali ya kufanyika kwa mkutano huo pia wamepata fursa ya kutembelea hifadhi ya ziwa manyara na lengo ni kutangaza vivutio vilivyopo.
"Mhifadhi napenda kukuhakikishia kuwa mara baada ya mkutano huu tumejipanga kutangaza hifadhi ya Manyara kupitia vyombo mbalimbali vya habari, hapa tuko waandishi zaidi ya 40 kwa hiyo tegemea kuona habari nyingi katika vyombo nyetu vya habari,"alisema
Katika mkutano huo Wanachama wa APC walikubaliana kufanya mabadiliko ya Katiba yao kwa kuwa na muundo mpya ambao utakuwa na bodi na secretarieti ya kuajiriwa.




No comments:
Post a Comment