![]() |
| Picha na Shakira Nyerere |
![]() |
| Mwenyekiti kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma Dolnad Majetii akisisitiza jambo Katika Baraza la Madiwani |
NA: Shakira Nyerere, MAIPAC
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanashirikiana na kuhakikisha suala la uboreshaji wa elimu na ufaulu linapewa kipaumbele ili wapande kutoka nafasi ya kuwa wilaya ya 10 waliyopata kitaifa katika 9 ya darasa la Saba la mwaka 2022.
Pia limeshauri madiwani kujenga utaratibu wa utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ili kupata mbinu za kuyatatua badala ya kutumia muda mwingi kulalamika.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Dolnad Mejetii alitoa rai hiyo wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Kuhusu ufaulu, alisema lazima kuwa na mipango mikakati ya kuhakikisha wanaongeza ufaulu, wasibwete na nafasi hiyo ambayo wameipata lazima watambue kuwa kazi bado ni kubwa na inawezekana kuongeza ufaulu zaifi.
Akizungumzia changamoto za wananchi, alisema kazi ya kiongozi si kulalamika Kwa kuwa anakuwa amebeba dhamana, hivyo anapaswa kutafuta ufumbuzi wa kila changamoto ili kuhakikisha eneo husika linakuwa na maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Bahi, Sterwart Masima alipendekeza katika kikao hicho Madiwani na watendaji wawe na utoaji wa taarifa kwa kina kwani ndio kikao pekee ambacho shughuli za maendeleo ya kata zinsfahamika na kuelezwa kwa kina.
"Wataalamu wa halmashuri nashauri nje na muundo mahususi wa uandishi wa taarifa hizo ili kupata taarifa zote muhimu zinazohitajika kwenye shughuli za maendeleo za kata kuepuka ukosekenaji wa taarifa,"alisisitiza.
Baadhi ya madiwali licha kuanisha changamoto mbalimbali zinakabili kata zao hasa kwenye elimu wameonesha kuridhishwa na upatikanaji wa fedha za shughuli za maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya elimu kama madarasa na vifaa kwa wanafunzi kwenye ngazi za shule ya msingi na sekondari kutoka kwenye mfuko wa elimu.
Wakizungumzia shule ambazo zina wanafunzi wenye mahitaji Maalum wakiwemo viziwe Kigwe na wale wa mtindio wa ubongo, walishauri ziangaliwe kwa jicho la karibu ili kupatiwa vifaa vya kujifunza na kufundishia na walimu wa taalam ili kuondokana na kushika nafasi ya mwisho katika ufaulu
Akiaga wajumbe wa baraza hilo na watumishi wa Bahi Mkuu wa wilaya Mwanahamis Mkunda anayehamishiwa wilaya ya Temeke aliwahimiza kuendeleza ari ya kazi aliyopo, kushirikiana na kuendeleza mafanikio ya elimu waliyoanza kuyapata.
Naye Mkuu wa Wilaya mpya wa Bahi Godwine Gondwe ameripoti rasmi wilayani humo akitokea wilaya ya Temeke baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza Wilaya hiyo huku aliahidi kuendelea kufanya kazi za mtangulizi wake Mwanahamis Mkunda anayehamishiwa wilaya ya Temeke.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), katika wilaya hiyo aliahidi kushirikiana kikamilifu na viongozi wenzie kutekeleza kikamilifu na kwa vitendo Ilani ya Chama kama alivyofanya Temeke.
"Namini Rais, Samia amepeleka Bahi kwa makusudi na atalifanyia kazi suala hilo kwa vitendo na kuleta tija, kama walivyoweza katika wilaya ya Temeke ambayo kwa mwaka 2022 ikiongoza na kushika nafasi ya kwanza Tanzania nzima,"alisema Gondwe


No comments:
Post a Comment