DC MPYA CHEMBA ALA KIAPO LEO AOMBA USHIRIKIANO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 30 January 2023

DC MPYA CHEMBA ALA KIAPO LEO AOMBA USHIRIKIANO

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Chemba Gerald Mongela

Mkuu wa Wilaya Mpya wa Chemba Gerald Mongela,Akila kiaopo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule

Mkuu wa Wilaya Mpya ya Chemba Mkoa wa Dodoma, Gerald Mongela akisaini kitabu Cha utambulisho wa uongozi

N: SHAKIRA NYERERE, Maipac

Mkuu wa Mkoa wa DODOMA Rosemary Senyamule amemuapusha Mkuu mpya wa wilaya Chemba mapema leo Januari 30.2023 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa  na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya mkoa na wilaya, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.


Akizungumza baada ya uapisho huo,RC Senyamule amewataka wakuu wote wa wilaya kuzingatia na kuheshimu viapo vyao vya utumishi na uadilifu..

."Nawakaribisha sana Dodoma,nawasisitiza mkaendelee kuzisoma kanuni za viapo vyenu ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yenu Kwa Serikali na wananchi"amesema Senyamule

Aidha amesisitiza swala la utawala Bora,kushughulikia kero za wananchi, ukusanyaji wa mapato, Ustawishaji wa Mazingira, Kushughulikia swala la Elimu bora hususani  swala la ufaulu na uandikishaji na upelekwaji wa wanafunzi wa darasa la awali,darasa la kwanza na kidato Cha kwanza.

Hafla hiyo pia  imehudhuriwa na Wakuu wa wilaya wote wa wilaya zingine za mkoa wa Dodoma ambao wameendelea kubaki katika vituo vyao vya kazi vya awali Kutoka wilaya za Dodoma Mjini, Kongwa, Chamwino, pamoja na Wakuu wa wilaya waliohamishiwa wilaya za Bahi na Mpwapwa

Akitoa neno la shukrani mara baada ya kula Kiapo hicho ,mkuu huyo Mpya wa wilaya ya Chemba amemshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Kumteua kuwatumikia wananchi na serikali wilayani Chemba.

Aidha amemwahindi mkuu wa Mkoa kuyafanyia kazi maelekezo yake yote na kwamba atafanya kazi Kwa kutumia karma, maarifa,ubunifu na Kwa kuzingatia kiapo chake.

Akizungumza Kwa niaba ya wakuu wa wilaya wote ,Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa aliyehamia Sophia Mfaume Kizigo amemwahidi mkuu wa mkoa utumishi unaozingatia maadili na kwamba Mkoa wa Dodoma ni tunu na fahari ya Watanzania na wao wako tayari Kuwa sehemu ya wanaoienzi na kuistawisha tunu.


No comments: