Shakila Nyerere, MAIPAC Doodma
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa, Muhsin Ussi amewahakikishia vijana wa Tawi la UVCCM CITY CENTRE kupatiwa mikopo ya pikipiki li wajiajiri na wajikwamue kiuchumi.
Tawi hilo limezinduliwa Leo Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma ambapo ufunguzi huo umefanyika sambamba na Sherehe za Kuadhimisha Miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania tangu kilipozaliwa Mwaka 1977.
Akizungumza na Vijana hao Muhsin Ussi Amesema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, inataka mapato ya Ndani ya Halmashauri yatenge Asilimia (10%) kwa ajili ya mikopo kwa vikundi, ambazo zimegawanywa katika Makundi Matatu,Asilimia (4%) kwaajili ya kundi la akina Mama,Asilimia (2%) Kundi la Vijana wenye uhitaji Maalumu na Asilimia (4%) Nyingine inawagusa Vijana moja kwa moja.
Kutokana na Asilimia (4%) ya Fedha iliyotengwa kwaajili ya Vijana, Ndg.Muhsin ametoa Ahadi ya kuwahakikishia vijana wa Tawi hilo kuwa Halmashauri inawapatia Fedha kwaajili ya kununua Bodaboda.
"Fedha hizi zimewekwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutatua Changamoto za Vijana Lazima Vijana wazipate Fedha hizi, Ikiwa kuna mtu yeyote alikuwa anatumia Janjajanja kukwepesha Fedha hizi zisiwafikie Vijana waliokusudiwa, Huyo mtu tunampa Salamu arobaini yake imefika".Amesema Ussi.

No comments:
Post a Comment