| Mtangazaji wa TBC Grace Henry Kingalame aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang’halwe mkoani Geita |
NA: ANDREA NGOBOLE, MMT
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 37, kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 48 na wengine 55 kubakia katika vituo vyao vya kazi.
Kati ya wakuu wa wilaya wapya 37 walioteuliwa, majina ya waandishi wa wa habari yemejitokeza katika wateule hao.
Miongoni mwao ni mtangazaji wa muda mrefu wa shirika la utangazaji nchini TBC, Grace Henry Kingalame aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang’halwe mkoani Geita, Kasilda Jeremia Mgeni Mwandishi mkoani Morogoro aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na Jaffar Mohamed Haniu mtangazaji wa muda mrefu TBC, alishafanya Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu na pia Mkurugenzi wa chanel ten, ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
| Jaffar Mohamed Haniu aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. |
Rais ameendelea kuwaamini Wakuu wa wilaya wenye taaluma ya habari ambao amewahamisha vituo vyao vya kazi na kuwapeleka maeneo mapya ya kazi ambao ni pamoja na Godwin Crydon Gondwe amehamishiwa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma akitokea wilaya ya Kinondoni mkoani Daresalaam, Fatma Almas Nyangasa aliyehamishiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani akitokea wilaya ya kigamboni mkoani Daresalaam na Simon Peter Simalenga aliyehamishiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Bariadi akitokea wilaya ya Songwe.
| Mwandishi na mtangazaji wa muda mrefu Godwin Crydon Gondwe amehamishiwa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma akitokea wilaya ya Kinondoni mkoani Daresalaam |
Aidha majina ya wakuu wa wilaya wenye taaluma ya habari ambao wameachwa katika uteuzi huu mpya ni pamoja na Jerry Muro aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambaye nafasi yake inachukuliwa na Thomas Cornel Apson aliyehamishiwa kutoka wilaya Siha mkoani Kilimanjaro, na Gabriel Zakaria aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Busega ambaye nafasi yake inachukuliwa na Anna Jerome Gidarya aliyehamishiwa kutoka wilaya ya Ileje.
| Mtangazaji wa habari maarufu, Gabriel Zakaria aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Busega, katika uteuzi huu ameachwa |
| Mwandishi na mtangazaji Nguli, Jerry Muro aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambaye naye katika uteuzi huu hajateuliwa. |
No comments:
Post a Comment