![]() |
| Katibu Tawala Mkoa wa DODOMA Dk. Fatuma Mganga akizungumza na wanahabari hawapo pichani |
SHAKILA NYERERE, MAIPAC DODOMA
KATIBU tawala Mkoa wa Dodoma Dk.Fatuma Mganga amefungua mafunzo ya program Shule Bora kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma wilayani Kondoa.
Amesema kuwa swala la Elimu katika Mkoa wa Dodoma bado halijatangazwa vizuri na kuwataka waandishi wa habari wakawe chachu cha kuielimisha jamii.
Amempongeza Rais Samia Sulluhu Hassan Kwa jitihada zake za dhati za kuongeza pesa za maendeleo katika mkoa wa Dodoma ambapo shilingi bilioni 7.8 zimetolewa na kuwezesha kujenga vyumba vya madarasa 393 ya shule za msingi na madarasa 130 yamejengwa Kwa shule za sekondari kwa gharama ya shilingi bilioni 20
Aidha amewaeleza waandishi wa habari kuwa Rais Samia ameongeza bajeti ya Elimu bila malipo Kwa shule za misingi na sekondari.
Pamoja na jitihada hizo za serikali amewataka wazazi kushirikiana na serikali katika ujenzi na uhifadhi wa Miundombinu ya elimu ikiwemo ya madarasa ambapo ameeleza Mkoa kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 7000 ,ambapo mwaka huu peke yake wanatarajia zaidi ya wanafunzi elfu 90 kuanza masomo.
"Ninawaomba wazazi wawapeleke watoto shule ,wasiwafiche na kuwatumikisha Shughuli za kilimo na kazi za ndani."Amesema Fatuma
Aidha amekemea dhana iliyozoeleka kwamba Mkoa wa Dodoma ni zao la wadada wa ndani kutoa House girl[Wasaidizi wa Shughuli za ndani]
Amesema Mpaka kufikia January 26.2023 ilifikia asilimia 89.7 ya wanafunzi wa madarasa la awali walioripoti shule,huku asilimia 94.2 Kwa darasa la kwanza na asilimia 66.95 kidato Cha kwanza
.."Nawaomba waandishi wa habari mkausaidie mkoa kutangaza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu mkoani kwetu,kuyatangaza mafanikio haya Kwa jamii yatarahisisha serikali kuendelea kutuunga Mkono katika jitihada zetu hizi."Alisema Fatuma
Fatuma akapongeza kwa kusema juu ya Matamanio ya mkoa ya mwaka huu 2023 ni kuwa na ufaulu wa asili 95 ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba na angalau asilimia 75 ya wanafunzi wanaohitimu kidato Cha Nne Wawe na ufaulu wa daraja la 1-3.
"Aidha ni matamanio ya mkoa kuondoa changamoto ya watoto kukaa chini Pamoja na wanafunzi wote watakaoshindwa mtihani wao wa darasa la saba kujiunga na vyuo vya ugundi stadi VETA"Amesema Fatuma
Naye mratibu wa Program ya shule Bora Mkoa wa Dodoma Mtemi Zombwe ametoa wito kwa wandishi kufanya kazi kwa kufuata Dira nne za Program zilizopo Katika shule Bora
Hata hivyo alisema watoto wa darasa la kwanza na lapili ili waweze kufikia malengo ya kujua kusoma na kuandika inahitajika amani kwakua anakua Katika umri mdogo hivyo linalohitajika nikupewa amani
![]() |
| Waandishi wa habari, pamoja na maafisa Habari Mkoa wa Dodoma wakiwa makini kumsikiliza Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Fatuma Mganga wakati akizungumza juu ya Program ya Serikali ya shule Bora |



No comments:
Post a Comment