|
Waziri
wa Fenda na Mipango, Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana
na Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Peter Mathuki kabla ya
kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), unaofanyika Jijini Bujumbura, Burundi |
|
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)
(kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) wakipitia nyaraka mbalimbali
wakayti wa Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), uliofanyika Jijini Bujumbura, Burundi. Wa tatu kushoto
ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi– Sekta ya ujenzi, Mhe.
Mha. Godfrey Kasekenya (Mb). |
|
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban
akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki
uliofanyika Jijini Bunjura nchini Burundi. Kushoto kwa Bi. Amina ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Joseph Edward Sokoine na anayefuatia ni Naibu Waziri wa Katika na
Sheria Mhe. Geoffrey Mizengo Pinda (Mb) |
|
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa
na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Yamungu Kayandabila
wakiwasili katika Hotel club du lac Tanganyika kuhudhuria Mkutano wa 43
wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini
Bujumbura nchini Burundi. |
Na. Ramadhani Kissimba, Bujumbura -Burundi
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameshiriki
katika Mkutano wa 43 wa kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya
Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Bunjura, Burundi. Mkutano huo ambao
umefanyika baada ya miaka nane (8) toka ulipofanyika kwa mara ya mwisho
nchini Burundi umeshirikisha Mawaziri wanaosimamia masuala ya Afrika
Mashariki na ushirikiano wa Kikanda pamoja na Mawaziri wenye agenda
zinazojadiliwa na Baraza hilo.
Awali
kabla ya Mkutano huo kulitanguliwa na vikao vya Wataalamu na Makatibu
Wakuu kutoka katika nchi wanachama vilivyofanyika kuanzia tarehe 19 – 22
Februari, 2023 ambao walipitia agenda na mapendekezo mbalimbali ya
Jumuiya. Aidha wataalamu hao walipitia taarifa ya utekelezaji wa
maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo ya
biashara, forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii,
ajira, utawala na fedha.
Dkt.
Nchemba ameshiriki Mkutano huo pamoja na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa
na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt.
Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambapo watajadili na kupitisha mapendekezo
ya agenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuitangaza lugha ya
Kiswahili kwa kuanzisha vituo vya utamaduni wa lugha hiyo katika Balozi
za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa muelekeo wa kuanza
kutumika kwa lugha ya Kiswahili na Kifaransa katika uendeshaji wa
shughuli rasmi za Jumuiya.
Mkutano
wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulikuwa
chini ya Uenyekiti wa Burundi na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchini
Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Rwanda na Sudan Kusini umemalizika tarehe 23 Februari, 2023 na maazimio
na agenda zilizopitishwa zitawasilishwa katika mkutano wa Marais wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuridhia utekelezaji wake.
No comments:
Post a Comment