BASSOTU SECONADRY, FEMA WAWAJENGEA WANAFUNZI UJASIRI NA KUJITAMBUA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 1 February 2023

BASSOTU SECONADRY, FEMA WAWAJENGEA WANAFUNZI UJASIRI NA KUJITAMBUA

Wanafunzi wakiwa katika mdahalo huo

Baadhi ya walimu wakipitia jarida la FEMA

Mdahalo ukiendelea shuleni hapo

Mkuu wa shule ya Sekondari Bassotu Wilayani Hanang'Mkoa wa Manyara, Alex Joseph Mwangesi akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo juu ya kulipokea somo la ujasiri wa kusimama mbele za watu na kuongea


 

Na Mwandishi wetu,Maipac Manyara 

Shule ya Sekondari Bassotu iliopo Wilayani Hanang' Mkoa wa Manyara imefanya zoezi la kuwajengea zoezi la ujasiri wa kusimama mbele za halaiki wanafunzi waliopo kwenye Clab ya FEMA Katika shule hiyo

Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa Shule hiyo Alex Joseph Mwangesi baada ya kutoa mafunzo ya ujasiri kwa vijana hao alisema wameona ni vema kumuandaa kijana angali akiwa shuleni ili atakapo hitimu elimu ya Sekondari awe nauwezo wa kujielezea

"Tumefanya hivi kwa kuwa tunaona Kuna baadhi ya vijana huko mitaani unapokwenda kwenye jamii hususani masuala ya Tasaf unakuta kijana anasaini kwa kutumia dole gumba ama anaomba mtu amsomee kwa kutokujisimamia mwenyewe. Pamoja na hayo sisi shulin hapa Kuna Clab ya FEMA inatupatia elimu kupitia majarida wanayotutumia. Hivyo sisi shule tumetenga muda wa siku Moja Katika juma lakuelimishana "amesema Alex

Kwa upande wake Wakala wa Jarida Mkoani Manyara Shakila Nyerere, amewapongeza vijana wa Clabu ya FEMA shule ya Bassotu kwa kujali na kuitumia Elimu wanayopelekewa kwa kupitia Jaria Hilo huku akwasisitiza suala la kujitambua na kuzingatia Elimu wanayofundishwa

"Niwaase wadogo zangu, Elimu mnayoipata mnapaswa kuzingatia , na kumshuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassani kwa kuipa  kipaumbele Katika idara ya Elimu, Leo kupitia yeye tunasoma Bure huku badhi ya makampuni kuwaongezea faida ya kujitambua , kama hivi mnavyopata Elimu ya ujasiria Mali, kujitambua Katika makuzi na wengine mnayoyapata kupitia FEMA"alisema Shakila

Akizungumza Kwa niaba ya wenzake Tumaini Yuda wa kidato Cha tatu amelishukuru shirika la FEMA kwa kuwapelekea majarida na kusema tangia ajiunge na Clab ya FEMA amejifunza vingi na ataendelea kujifunza

"Najifuarahia kwa maamuzi ya kujiunga na Clab ya FEMA hapa shule, Kila jarida linapofika basi napenda soma na najifunzaambo engi. Nawashukuru FEMA kwa huu mradi na hata wanaotuletea Hadi shule"amesema yuda.

No comments: