Rais Samia afanya mabadiliko, Baraza la Mawaziri, Wizara ya Maliasili na Utalii " bado kaa la moto" kwa Mawaziri - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 14 February 2023

Rais Samia afanya mabadiliko, Baraza la Mawaziri, Wizara ya Maliasili na Utalii " bado kaa la moto" kwa Mawaziri

Mheshimiwa Mohamed Omar Mchengerwa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

Balozi Dkt. Pindi Chana ameteuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo

 

Mwandishi wetu, Maipac 
maipacarusha20@gmail.com


Rais Samia Suluh Hassan amefanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri na kuigusa tena Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari,Leo jioni iliyotolewa na  Mkurugenzi ya mawasiliano Ikulu imesema kuwa Rais amemteua  Mohamed Omar Mchengerwa,aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kahamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mwasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amehamishiwa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.


Rais Samia amemteua Dkt. Hassan Abbas aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Nafasi huyo ilikuwa inashikiliwa na Profesa Eliamani Sedoyeka.


Rais amemteua Bw. Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuchukua nafasi ya Dkt. Hassan Abbas Said aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Yakub alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Wateule Hawa wataapishwa tarehe 15 February 2023 saa 10.00 jioni Ikulu Dar es Salaam.

Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Sasa unaweza kusema ndio Wizara ngumu zaidi kudumu kwa Mawaziri wake pamoja na Makatibu wakuu.


 

 

No comments: