NAIBU KATIBU MKUU MPYA MALIASILI NA UTALII APOKEWA KWA SHANGWE NA MENEJIMENTI YA WIZARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 28 February 2023

NAIBU KATIBU MKUU MPYA MALIASILI NA UTALII APOKEWA KWA SHANGWE NA MENEJIMENTI YA WIZARA


Kikao Cha ukaribisho kikiendelea

Baadhi ya a watendaji wa Wizara hiyo 

Picha ya pamoja na Naibu KATIBU Mkuu mpya

Naibu KATIBU Mkuu mpya , Anderson Mutatembwa akipokewa na manejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma mapema leo



Na: Mwandishi wetu, Dodoma


maipacarusha20@gmail.com


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, amewaongoza menejimenti na wafanyakazi wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Katibu Mkuu mpya , Anderson Mutatembwa aliyeapishwa jana Ikulu.


Mapokezi haya yamefanyika Leo February 28,2023 ofisi za Wizara hiyo Mtumba Dodoma licha ya mapokezi hayo, Dkt. Abbasi amewaongoza wafanyakazi hao kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Juma Selemani Mkomi aliyeapishwa jana kuwa Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais Utumishi.


“Leo tunapokutana hapa kumuaga Bw. Mkomi na kumkaribisha Bw Muta labda mfahamu tu sisi watatu hapa tunafahamiana siku nyingi na kubwa wote tulikuwa katika Timu iliyoratibu kwa mafanikio makubwa ushiriki wa Rais wetu . Dkt. Samia Suluhu Hassan katika filamu ya Royal Tour na sote tulizunguka na Rais nchi nzima kwa hiyo tunaufahamu mkubwa wa jinsi ya kuutangaza utalii kwa kiwango kikubwa,” amesema Dkt. Abbasi.


Kwa upande wake Katibu Mkuu Mkomi amewashukuru wafanyakazi hao kwa ushirikiano mkubwa waliompa akiwa Wizarani hapo huku . Muta naye akiahidi kujifunza haraka ili kazi iendelee na kuomba ushirikiano wa wafanyakazi wote..


Wizara hiyo pia imepata Waziri wa Maliasili na Utalii mpya Mohamed Mchengerwa ambaye amechukuwa nafasi ya Dk Pindi Chana ambaye amehamishiwa Wizara ya Utamaduni na Michezo.


Dk Abbas ameteuliwa kuchukuwa nafasi ya Profesa Eliamani Sedoyeka ambaye atapangiwa majukumu mengine.


No comments: