NEHEMIA MCHECHU ATEULIWA KUWA MSAJILI HAZINA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 24 February 2023

NEHEMIA MCHECHU ATEULIWA KUWA MSAJILI HAZINA

 

Nehemiah Mchechu aliyeteuliwa kuwa Msajili wa Hazina 

Na Andrea Ngobole, Maipac

maipacarusha20@gmail.com

Rais Samia Suluh Hassan  Amemteua Nehemiah Kyando Mchechu kuwa Msajili wa Hazina. 

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni hii na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa uteuzi huo unaanza Leo.

Kabla ya uteuzi huo  Nehemiah Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

 Mchechu anachukua nafasi ya Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Rais pia amemteua Hamad Abdallah kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kabla ya uteuzi huo Hamad alikuwa Mkurugenzi mtendaji wa Gimcoafrica limited na anachukua nafasi ya Nehemiah Mchechu aliyeteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

Amemteua Mussa Mohamed Makame kuwa mkurugenzi mtendaji shirika la Maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC).

Kabla ya uteuzi huo Makame alikuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Maendeleo ya petrol Tanzania na pia ni mshauri mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania.

Makame anachukua nafasi ya Dkt.James Matagio ambaye atapangiwa kazi nyingine

Uteuzi huo ni kuanzia Leo tarehe 24/02/2023






No comments: