NA: MWANDISHI WETU, BABATI
Wakazi wawili wa kijiji cha Endagire wilayani Babati
mkoani Manyara wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani kila mmoja baada ya kutiwa
hatiani kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo bila ya uwa na kibali cha
uwindaji.
Waliohukumiwa kifungo hicho na mahakama ya wilaya hiyo
ni John Lulu (42) na Zebedayo Safari (34)
Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo jana, Hakimu Mkazi
Mfawidhi Victor Kimario alisema washtakiwa hao wametiwa hatiani kwa kosa la
kumiliki kinyume cha sheria meno mawili ya tembo ambayo ni nyara ya serikali.
Hakimu Kimario alisema kuwa washtakiwa hao walitenda
kosa hilo Octoba 23 mwaka 2022 wakiwa katika kijiji cha Burukeli wilaya ya
Babati.
Katika hukumu hiyo alisema washtakiwa hao walikamatwa
wakiwa wanasafirisha vipande viwili vya meno ya tembo yenye thamani ya shilingi
million 35.1 ambayo ni sawa na tembo mzima.
“Baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka
uliowasilisha vielelezo tisa ambavyo vilithibitisha mahakama hiyo kuwa
washtakiwa walikutwa na nyara za serikali na kisha kusikiliza upande wa utetezi
mahakama imejiridhisha pasipo na shaka kwamba walitenda kosa hilo.”
“Kutokana na kosa hilo mahakama hii inawatia hatiani
kwa kukiuka kifungu cha 86 (1) (2) (b) cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori
sura ya 283 ya sheria iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Kabla ya kusomwa hukumu hiyo wakili wa serikali
Rusticus Mahundi akisaidiwa na wakili Abood Komanya alidai mahakamani humo kuwa
washtakiwa hawana rekodi ya kufanya makosa ya uhalifu ila kwa kiwa Wanyamapori
wana mchango mkubwa katika pato la Taifa ni vyema mahakama hiyo ikawapa adhabu
wanayostahili iwe fundisho kwa watu wengine.
No comments:
Post a Comment