ASKARI NA KARANI WA MAHAKAMA WAFA AJALINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 5 March 2023

ASKARI NA KARANI WA MAHAKAMA WAFA AJALINI

 

Gari liliopata ajali na kusababisha VIFO kwa askari Polisi 


NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC CHALINZE



WATU watatu wakiwemo Askari polisi wawili wamefariki dunia kwenye ajali iliyotokea huko Mboga Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Machi 05 majira ya saa 11:45 alfajiri huko maeneo ya mavi ya Ng'ombe, Kijiji cha Mboga, Kata ya Msoga, Tarafa ya Chalinze, Wilaya ya Kipolisi Chalinze.

 Kamanda Lutumo alisema, gari lenye namba za usajili T.323 BAL aina ya Toyota Crester likiendeshwa na mkaguzi msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani (28), askari wa kituo cha Polisi Chalinze, akitokea Chalinze kuelekea Lugoba, liliacha njia kutoka upande wa kushoto 
wa barabara na kwenda upande wa kulia na kugonga karavati kisha gari hilo kupinduka na kusababisha vifo vya watu wa tatu.

Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani, Konstebo Emmiliana Charlse (26) askari Polisi kituo cha Polisi Chalinze na Karimu Simba (27) aliyekuwa karani wa mahakama ya Wilaya ya Lugoba.

Kamanda Lutumo alisema majeruhi wa ajali hiyo ambaye ni Polisi Konstebo Mwanaidi Shabani  (25) askari wa Kituo cha Polisi Chalinze  amebainika kuumia maneneo mbalimbali ya mwili wake na amepelekwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Uchunguzi wa awali umebaini, Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva kushindwa kulimudu gari na kupinduka na kusababisha vifo hivyo, majeruhi mmoja na uharibifu wa gari hilo.

No comments: