Dkt. JAFO AISHUKURU SERIKALI KWA VIFAA TIBA HOSPITAL YA WILAYA YA KISARAWE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 29 March 2023

Dkt. JAFO AISHUKURU SERIKALI KWA VIFAA TIBA HOSPITAL YA WILAYA YA KISARAWE

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu WA RAIS  Muungano na Mazingira Dkt. Seleman Jafo akizungumza wakati WA makabidhiano ya Vifaa Tiba mbalimbali kwa Uongozi wa Hospital ya Wilaya ya KISARAWE.




Baadhi ya vitanda vilivyokabidhiwa hospitalini hapo


NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KISARAWE



WAZIRIwa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira (Mb) jimbo la Kisarawe Dkt. Selemani Said Jafo  amekabidhi vifaa mbalimbali vya afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuboresha huduma za afya katika wilaya hiyo Kwa Vijiji 66.

Katika makabidhiano ya vifaa hivyo Dr Jafo amewapongeza watendaji wa Idara ya  afya katika hospitali hiyo kwa kazi wanayofanya katika kuwahudumia wagongwa na pia ameahidi kuwa nao karibu ili kutatua baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

Waziri huyo amepongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa namna inavyotatua vikwazo vya Wilaya ya  Kisarawe ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa Huduma ya Afya Kwa kuipatia Vifaa Tiba na fedha mbalimbali Kwa Ajili ya Afya ambayo inaifanya Halmashauri hiyo kuwa imara katika Huduma za Afya.

Aidha wananchi walioshiriki mapokezi ya vifaa hivyo wameishukuru serikali kwa kwa hatua hivyo wakidai vitapunguza usumbufu wa upatikanaji wa huduma ya matibabu hospitalini hapo

No comments: