EFTA na CRDB waja na mkakati kusaidia sekta ya Kilimo nchini - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 20 March 2023

EFTA na CRDB waja na mkakati kusaidia sekta ya Kilimo nchini

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Janeth Mayanga akijaribu moja ya matrekta ya New Holland TT 75 ambayo wananchi wa wilaya yake wananufaika nayo kwa kuyapata kupitia mikopo isiyokuwa na dhamana kutoka taasisi ya EFTA.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Janeth Mayanga akijaribu moja ya matrekta ya New Holland TT 75 ambayo wananchi wa wilaya yake wananufaika nayo kwa kuyapata kupitia mikopo isiyokuwa na dhamana kutoka taasisi ya EFTA.

 
Baadhi ya Wakulima wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya 


Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Bi Janeth Mayanja akizungumza na Wakulima wilayani Hanang'



.wakulima Mkoa Manyara waanza kunufaika.


Mwandishi wetu, MAIPAC Manyara

maipacarusha20@gmail.com


Katika kuhakikisha wakulima nchini wanalima kwa kutumia zana za kilimo za kisasa na zinakazochochea ufanisi katika uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali ya kilimo na kuwa na hazina ya kutosha ya chakula taasisi ya EFTA na benki ya CRDB waja na mkakati kuwasaidia wakulima.


Hayo yamebainika katika mafunzo yaliyoandaliwa na EFTA na Benki ya CRDB pamoja na wauzaji wa Matrekta ya New Holland kupitia kampuni ya Hughes Agriculture Tanzania kuhimiza matumizi ya zana za kisasa za kilimo, utunzaji wa kumbukumbu na matumizi ya fedha.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya kwanza kwa wakulima wa Hanang ambayo yalifanyika katika mji wa Katesh, Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Janeth Mayanja amesema ili wakulima waweze kulima kwa ufanisi ni lazima serikali kwa kushirikiana na taasisi binafsi zishirikiane kutengeneza mazingira Rafiki yatakayo wezesha mkulima kuziona fursa mbele yake.


“Kwa Hanang zipo fursa nyingi sana za kilimo, na hii imechangiwa na uwepo wa ardhi inayokubali karibu mazao yote kwa kila msimu na hivyo kuongeza chachu kwa wakazi wa hapa kujihusisha na Kilimo.” amesema 


Mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa licha ya ardhi bora kwa kilimo ila upatikanaji wa elimu ya mara kwa mara ihusuyo masuala ya kilimo imekuwa pia ni chachu ya kuwafanya wakulima kulima kilimo bora zaidi.


“Utaona umati huu mkubwa hapa, haujaja tu, wako hapa kuchota maarifa yatakayosaidia kuongeza ufanisi wao shambani” amesema


Na ndio maana kwa niaba ya uongozi wa Mkoa ninawashukuru sana wadau wetu hawa wa EFTA pamoja na washirika wao kwa mafunzo haya.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA, Bwana Nicomed Bohay amesema sambamba na mafunzo juu ya matumizi ya mashine katika kilimo, taasisi yake imewaletea pia wakulima wa Hanang na mkoa wa Manyara kwa ujumla wake, mikopo ya mashine na hasa matrekta ya New Holland ambayo yatakuwa yakipatikana kwa mkopo kwa wakulima bila dhamana.


Bohay ameongeza kuwa kwa sababu wakulima wengi walikuwa hawakopesheki, taasisi EFTA kupitia mkakati wake ilikuja na mpango wa mikopo ambayo haina dhamana ili kutoa fursa nyingi zaidi kwa wakulima kuweza kukopesheka mashine za kilimo.


Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa licha ya kuondoa kipengele cha dhamana lakini pia wamewarahisishia wakulima namna ya kulipa.


“Wakulima wetu hawa wanategemea kilimo na kilimo siyo shughuli ya kwamba utalima leo na kesho utaanza kuziona hela, Ili mkulima aanze kunufaika na kilimo anahitaji muda ili mazao yakomae mpaka kufikia hatua ya mavuno, na sisi tumeweka utaratibu kuwa marejesho ya mikopo ya wakulima yatakuwa yakifanyika wakati wa mavuno au misimu kwa kipindi cha hadi miaka mitatu ili kutoa nafasi kwa wakulima kupata pesa baada ya kuuza mazao yao ili kufanya malipo.” Amesema Bohay


Kwa upande wao baadhi ya wakulima wamesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati na yatawasaidia kuongeza ubunifu katika shughuli zao za kilimo.


Mkulima John Samweli alisema ,wanategemea kilimo maana asilimia karibu 90 ya watu wa Hanang ni wakulima lakini changamoto tuliyonayo licha ya kuwa na maeneo makubwa ya kulima bado hawanauwezo wa kumiliki mashine nyingi za kilimo kwa wakati mmoja .


"hali inatuanya tusiweze kulima maeneo makubwa, na hii inasababishwa na bei kubwa ya mashine hizi ambazo wakulima wengi hatuwezi kulipa mara moja"alisem




Hata hivyo tunawashukuru sana EFTA maana kupitia wao sasa tunao uhakika tutaweza kumiliki matrekta zaidi na tutaongeza maeneo zaidi ya kilimo na kupata mavuno zaidi.

No comments: