WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WAMPONGEZA RAIS SAMIA KULIPONYA TAIFA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 21 March 2023

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WAMPONGEZA RAIS SAMIA KULIPONYA TAIFA

 

Mratibu wa kitaifa wa THRDC Wakili Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza na vyombo vya habari


Mratibu wa kitaifa wa THRDC Onesmo Ole Ngurumwa


Mwandishi wetu, Maipac

maipacarusha20@gmail.com


Mtandao wa watetezi wa haki za Binaadamu (THRDC) umeeleza mambo mazuri ambayo amefanya Rais Samia Suluhu katika miaka yake miwili ya uongozi na kubwa kuliponya Taifa na majeraha ya ukiukwaji wa haki za Binaadamu.



Mratibu wa kitaifa wa THRDC Onesmo Ole Ngurumwa ametaja mambo sita makubwa  ambayo kimsingi yaligusa sana sekta ya NGOs Tanzania, sekta binafsi na Maisha ya Watanzania kwa ujumla wake. 


Ole Ngurumwa amesema  NGOs za utetezi wa haki za binadamu zilibanwa kwa kuwekewa vikwazo, ikiwemo mtandao wetu wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania( THRDC) kwa kufungiwa akaunti zake zote kuanzia August 2020 hadi April 2021.


Hali iliyo pelekea miradi yote ya utetezi wa haki za binadamu iliyopangwa kwa mwaka 2020 kutokufanyika na kutuathiri mfumo mzima wa utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. 


Kwa namna ya pekee sana tunaungana na Mratibu wa THRDC Taifa kusema hakika Rais Samia ameliponya Taifa. 


 KUBORESHA NA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYA BIASHARA.


Tunaungana na Mratibu kusema yakua kwa namna ya pekee sana, ndani ya miaka miwili hii hali ya wafanya biashara imekua ni yenye kuruhusu kuendesha biashara zao kwa uhuru na uendelevu mkubwa hii ni pamoja na kutengenezewa mazingira wezeshi zaidi.


Kutoka  kwa watetezi tunaongezea katika kauli ya mratibu, kwa kusema hali hii imewezesha makusanyo ya kodi kwa taarifa ya TRA kuongezeka zaidi, ambapo Makusanyo ya Desemba 2022 yanatajwa kuwa na ufanisi wa asilimia 106.5, sawa na ukuaji wa asilimia 10.3 ukilinganisha na makusanyo ya Desemba 2021.


 UHURU WA VYOMBO VYA HABARI. 


Ni dhahiri kabisa yakua  sote tunafahamu namna ambavyo vyombo vya habari vimekua huru, hii ni kufuatia agizo la Mh.Rais la 06/04/2021 alipo agiza vyombo vya habari vifunguliwe, ambavyo baadhi ni gazeti la Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na Mseto. 

Hii ndio Maana halisi ya Mratibu wa THRDC na watetezi  kusema Mh.Rais, Dr Samia, ameliponya Taifa.


 KUKUA KWA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA. 


Hili bila kuhitaji Ufafanuzi mkubwa, Sote ni mashahidi wa ni kwa namna gani nchi yetu imekua na mabadiliko makubwa katika demokrasia leo hii UWT na BAWACHA wanacheka pamoja, Rais chama tawala anasindikizwa na wafuasi wa chama pinzani kwa furaha, si hivyo tu, hata vyama ambavyo havijapata fursa au havijahitaji kukutana na Mh.Rais, wao pia bado wako huru kufanya mambo yao ya kisiasa bila mipaka. 


Hii ndio maana ya MRATIBU THRDC na sisi watetezi kuungana naye kusema Mh.Rais, Ameliponya Taifa.


KUPUNGUA KWA MATUKIO YA KUKAMATWA NA KUPOTEA KWA WATU WALIOKUA MSTARI WA MBELE KUIKOSOA SERIKALI. 


Tunafahamu wote yaliyo mkuta Mh.Tundu Antipas Lissu, Lema pamoja na waandishi wa habari/ watetezi/wanaharakati kupotea, kukimbia,kuteswa na kutishiwa.  Lakini leo hii Mh.Rais anasema wanangu njooni nyumbani. 


Tunaungana na mratibu wa THRDC kusema hakika Mh.Rais ameliponya Taifa. 


 MH.RAIS DR. SAMIA SULUHU HASSAN AMEKUA MTETEZI NUMBER MOJA WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI TANZANIA. 


Kwa mara ya kwanza Tanzania, 13.05.2022 Mh.Rais alikutana na timu ya watetezi wa haki za binadamu katika maadhimisho ya miaka 10 ya THRDC na kuahidi kuendelea kushirikiana nasi akiwa kama mtetezi namba moja wa haki za binadamu Tanzania. 


Pia tunafahamu yakua tayari tuna TUME YA RAIS YA KUBORESHA HAKI JINAI iliyoanzishwa ili kuboresha mifumo yote ya haki jinai katika taasisi za serikali iwemo Polisi, Magereza, Takukuru,Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Uhamiaji na tume ya kudhibiti madawa ya kulevya ambapo mfumo wa maboresho unafanyika kwa kupokea maoni mbali toka kwa wadau na wananchi, THRDC ni moja ya wadau tulioshiriki kikamilifu katika kutoa maoni haya. 



No comments: