Wakili Joseph Shangai Akizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya mahakama kuu Kanda ya Arusha leo |
Mwandishi wetu, Maipac
maipacarusha20@gmail.com
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imetoa amri ya kufika mahakamani kwa wajibu maombi kwenye kesi ya kulazimishwa kupotea ( Enforced disappearance), kwa mzee Oriais Oleng’iyo, (85) wa Ololosokwan, Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro
Aidha kesi hiyo iliyokuja mahakamani kwa ajili kusikilizwa leo machi 22, mwaka 2023 ilishindwa kuendelea kutokana na mawakili wa wajibu maombi (Jamhuri ) kutoonekana mahakamani hapo.
Amri hiyo ilitolewa na Jaji Mohamed Gwae anayesikiliza maombi hayo namba 68/2022 ambapo wajibu maombi kwenye shauri hilo ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, , Mkuu wa mkoa wa Arusha , Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Arusha, , Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro na Mkuu wa polisi wilaya ya Ngorongoro.
Alisema anatoa siku chache kwa wajibu maombi kufika mahakamani huku akiwaagiza mawakili wa waleta maombi, Joseph Shangai, William Ernest na Simon Mbwambo kuja na mteja wao ambaye ni mtoto wa Mzee anayedaiwa kutoonekana.
Tangu kukamatwa kwa wananchi wapatao 19 wa loliliondo ambapo wengine walishafikishwa mahakamani na kesi yao kufutwa kasoro mzee Oriais Oleng'iyo ambaye hadi sasa inadaiwa hajulikani alipo.
Jaji Gwae aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 30 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa
Upande wa waleta maombi wanaiomba mahakama hiyo iamuru wajibu maombi kumleta mahakamani Oriaisi Ng’iyo ambaye amepelekwa kusikojulikana tangu alipokamatwa nyumbani kwake Engong’u Nairowa, Kata ya Ololosokwan, Loliondo wilaya ya Ngorongoro
Pia wanaiomba Mahakama iamuru au kuwaelekeza wajibu maomnbi kumwachia huru Oriasi Pasilange Ng’iyo Kurosawa alikoshikiliwa tangu Juni 10, 2022 na iamuru walalamikiwa waje mahakamani kueleza sababu za kumshikilia Oriasi Pasilange Ng’iyo kinyume cha Sheria.
Katika ombi lingine wanaoimba mahakama iamuru na kuelekeza wajibu maombi kuleta mwili wa Oriaisi Ng’iyo akiwa hai au asipokuwa hai
No comments:
Post a Comment