MHE. MCHENGERWA AZINDUA BOTI YA KISASA YA UTALII - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 15 March 2023

MHE. MCHENGERWA AZINDUA BOTI YA KISASA YA UTALII








 


👉Atoa wito kwa wananchi kuitumia


Na John Mapepele

maipacarusha20@gmail.com

Serikali imewataka wananchi wote nchini kutumia boti ya kisasa ya Utalii  iliyozinduliwa rasmi leo ili kukuza utalii wa ndani.


Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa  Kilwa Masoko kwenye hafla ya uzinduzi wa  boti  maalum ya Utalii ijulikanayo kama  TAWA SEA CRUISER  inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).


Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa  boti hiyo itakuwa ikifanya safari katika ukanda  wote wa Pwani ili wajionee vivutio mbalimbali vya utalii.


Amevitaja baadhi ya vivutio  vya utalii vinavyopatikana  katika eneo la Kilwa kuwa ni pamoja na misitu ya matumbawe, kasa, mikoko, na samaki wa aina mbalimbali.


Katika hatua nyingine  Mhe. Waziri ametembelea maeneo  ya kitalii ya mji mkongwe wa kihistoria wa Kilwa  na kujionea  vivutio vya utalii vya asili kama msikiti wa Karne ya 12  magofu ya kale na jumba la mfalme.


Akiwa katika msikiti wa kale ameiagiza Bodi ya TAWA  kuona namna ya kuboresha mji huo ili

 kuvuta watalii wengi.


#tanzaniaunforgettable #tanzaniaroyaltour

No comments: