TAKUKURU PWANI YAANGAZIA AMCOS - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 29 March 2023

TAKUKURU PWANI YAANGAZIA AMCOS

 




NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA

maipacarusha20@gmail.com 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani  imefanya ufuatiliaji  kwenye Vyama vya Ushirika vya Ushirika Vya Msingi vya Mazao na masoko (AMCOS) na kubaini uwepo wa udanganyifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo la udanganyifu wa kilo.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani Christopher Myava ameyabainisha hayo alipokua akizungumza na waandishi wa Habari alipokuwa akitoa taarifa ya miezi mitatu.

Akizungumzia kuhusu uchambuzi wa mifumo amesema kuwa ili kudhibiti mianya ya rushwa katika Idara za Serikali na sekta binafsi chambuzi za mifumo tatu zimefanyika kwenye maeneo ya uendeshaji na usimamizi wa masoko ya biashara pamoja na utekelezaji miradi kwa kutumia 'force account' 

Amesema uchambuzi huo umefanyika katika AMCOS za Mkongo Kilimani, Kitupa, Nyaminywili, Kipo na Ngorongo AMCOS zote za Wilayani Rufiji.

Myava amesema kuwa katika uchambuzi huo wamebaini kuwepo kwa udhaifu katika utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za Vyama vya Ushirika ambapo baadhi ya nyaraka zimekuwa zikitunzwa nyumbani kwa viongozi wa bodi huku akiitaja AMCOS ya Kipo kuwa baadhii ya nyaraka zake zimeonekana kuharibiwa na mchwa.

Amesema hatua ya kukosa kumbukumbu na nyaraka zilizoharibika inasababisha vikwazo kubaini mapato na matumizi takwimu na taarifa za fedha kwa ujumla.

Mkuu huyo wa TAKUKURU ameeleza kuwa katika AMCOS zilizofanyiwa uchambuzi wa mfumo upo udanganyifu wa kutoandika idadi ya kilo sahihi kulingana na mzigo wa mkulima katika upimaji kwa kisingizio cha ubora na unyaufu.

"Mfano Mwananchi anafika na kilo 30.5 lakini kwa makusudi ya kufanya udanganyifu wapimaji ambao ni wajumbe wa bodi ya AMCOS watamwambia mkulima mazao yako hayana ubora hivyo badala ya kilo 30.5 tutakadiria kilo 29" 

Hali hii ikiendelea kwa wakulima zaidi wajumbe hao watajikusanyia kilo nyingi kwa udanganyifu na kutengeneza mauzo kwa majina hewa" amesema Mkuu huyo wa TAKUKURU. 

Amebainisha kuwa wananchi wanapobaini udanganyifu huacha kuuza mazao kwenye AMCOS  zao na kwenda kuuza kwenye AMCOS  za jirani jambo ambalo linasababisha AMCOS mama zinakosa mapato.

Myava ameeleza maazimio yaliyowekwa kuwa ni kuwa na ujenzi wa Ofisi bora ya kutunza nyaraka na kumbukumbu za Ushirika uwe umekamilika ifikapo mwaka 2024, kuandaa taarifa za fedha na kujaza taarifa sahihi katika nyaraka zote za Ushirika na kuhakikisha zinatunzwa vizuri.

No comments: