WAOMBA MGODI WA TANZANITE GEM AND ROCK VENTURE UFUNGULIWE UANZE UZALISHAJI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 17 March 2023

WAOMBA MGODI WA TANZANITE GEM AND ROCK VENTURE UFUNGULIWE UANZE UZALISHAJI

 




Na: Mwandishi wetu, Mererani


maipacarusha20@gmail.com


Sakata la  vurugu zilizoibuka ndani ya Mgodi wa Tanzanite wa kampuni ya Gem and Rock Venture unaomilikiwa mfanyabiashara maarufu, Joel Saitoti ,limechukua sura mpya mara baada ya meneja wa mgodi huo,  kuibuka na kudai kuwa ezekiel isack akiwa na watu zaidi ya 30 waliwavamia na kuwashambulia kwa kipigo na kisha kunyang'anya madini kinyume cha sheria.


Akitoa ufafanuzi wa sakata hilo,  UFUlililotokea machi 13 mwaka huu,meneja wa mgodi huo Martin Msigwa alidai kuwa siku ya tukio wakiwa wanaendelea na uzalishaji wa madini hayo askari hao wakiwa ameambatana na wachimbaji waliwavamia na kuanza kuwapiga wafanyakazi wa kampuni hiyo wakilazimisha watoe madini waliokuwa wamezalisha zaidi ya kilo nne.


Alisema kabla ya askari hao kufika, alikuja mkaguzi wa baruti, Ezekiel Isaac ambaye alifanikiwa kuvunja geti la Mtobozano akipitia mgodi wa Franone Mining  na kuingia kitalu B inayomilikiwa na  kampuni ya  Gem and rock  bila kufuata taratibu .


"Baada ya kufika walikuta shughuli za uzalishaji zikiendelea na kutaka wapatiwe madini wakilazimisha yapitie mgodi wa Kitalu C,lakini vijana wetu waligoma kuachia madini hayo wakidai sio utaratibu wa kawaida kwakuwa mkaguzi wa baruti alikuwa mwenyewe alishirikiana na wafanyakazi wa Franone ,bila kuwepo askari polisi,jeshi la wananchi (JWTZ) na usalama wa taifa kama ilivyozoeleka"


Naye meneja msaidizi wa mgodi huo,Enock Nanyaro alidai kuwa kabla ya tukio hilo Machi 10 mwaka huu majira ya saa 10 jioni alipokea barua iliyotumwa kupitia mtandani wa WhatsApp kutoka kwa afisa mkaguzi wa baruti Ezekiel Isaac kwenda kwa meneja Nanyaro ikiitaka kampuni hiyo kusimamisha uzalishaji katika Kitalu B ili kupisha uchunguzi baada ya kuwepo malalamiko ya kuwepo kwa hewa chafu inayotokana na mlipuko wa baruti.




Nanyaro alisema kuwa  uongozi wa mgodi huo uliamua kujibu barua hiyo kwa njia hiyo hiyo ya whatsup wakimweleza Mkaguzi huyo kuwa umbali waliopo ni zaidi ya mita 580 kutoka mgodi wa Franone kwa hiyo sio kweli kwamba moshi wa baruti unawafikia.


"Tunashangaa kuona kampuni ya Franone wakilalamika kuhusu moshi wa baruti wakati wapo umbali mkubwa na sisi kama ni hivyo kwanini migodi mingine ya jirani kama mgodi wa Deo Minja ,Sunday na Papaking hawalalamiki"???


Naye  Wilbart Mosses mfanyakazi wa mgodi huo wa Gem and Rock Ventures amesikitishwa kuona mkuu wa usalama Mererani (DCO) kutoa amri kwa askari aliokuwa ameongozana nao kuanza kuwashambulia kwa kipigo kikali na kupokonywa madini yetu ambayo ndio ujira wetu na kuondoka nayo.


Mosses alimwomba rais Samia Sulluhu Hasan kuingilia kati sakata hilo ili kupata haki yao ya msingi kwani wamechoka kuonewa mara kwa mara pindi wanapoanza uzalishaji wa madini.




No comments: