WATANZANIA WAASWA KUTHAMINI UTAMADUNI WA JAMII ZAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 12 March 2023

WATANZANIA WAASWA KUTHAMINI UTAMADUNI WA JAMII ZAO

 





 Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza katika tamasha la Holi Milan 2023



Na Mwandishi wetu


maipacarusha20@gmail.com


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewaasa Watanzania kuheshimu, kuthamini  na kujivunia  utamaduni wa jamii zao.


Mhe. Pindi Chana amesema hayo leo  jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha  la Holi Milan 2023 la kusherehekea miaka 75 ya Uhuru wa India, ambapo ametumia nafasi hiyo kuwapongeza  wananchi wa India kwa kutumiza  miaka 75 ya Uhuru wao.


"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya  Tanzania na India uliodumu tangu uhuru ili kuhakikisha kuwa, shughuli za Utamaduni na Sanaa baina ya nchi hizi mbili zinaendelea kukua na kuwa chanzo cha mapato kwa wananchi wa Mataifa yetu mawili"


Balozi Dkt. Pindi ameeleza kuwa tamasha hilo linafundisha watu kuheshimu na kuthamini Utamaduni wao  akiwaasa Watanzania na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla  hiyo wapende na wajivunie utamaduni wao ambao umekua chanzo kikubwa cha kuleta mabadiliko chanya ya kupenda kufanya kazi na kushirikiana na watu mbalimbali.


" Tanzania na India tumekua na ushirikiano wa miaka mingi, tumeshuhudia nchi zetu zikishirikiana katika masuala mbalimbali ya afya, elimu, utamaduni, michezo na biashara.




Aidha, Balozi Dkt. Pindi Chana ameupongeza Ubalozi wa India kwa kuandaa tukio hilo muhimu hapa nchini akisisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.


Tamasha hilo limehudhuriwa na mabalozi na viongozi  mbalimbali na  kupambwa na burudani, Sanaa na Utamaduni wa Tanzania na India  wenye kuonesha hostoria ya  Mataifa hayo mawili.




No comments: