SEKONDARI YA VIZIWAZIWA KUANZA KUPOKEA WANAFUNZI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 5 April 2023

SEKONDARI YA VIZIWAZIWA KUANZA KUPOKEA WANAFUNZI

 


NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA



SHULE ya Sekondari Viziwaziwa inayojengwa Kata ya Viziwaziwa Halmashauri ya Mji Kibaha kupitia Secondary  Education Quality Improvement Project (SEQUIP) umefikia asilimia 97 ya ujenzi huku sh. Mil 540 zikitumika.

Tayari miundombinu yote ikiwemo Madarasa  nane,Maabara tatu  za sayansi, maktaba,chumba cha TEHAMA,Jengo la utawala,matundu ya vyoo 20 pamoja na miundombinu ya Maji ikiwa imeshafikia Kiwango cha kuwaruhusu wanafunzi 230 kuanza masomo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa  fedha iliyoidhinishwa na Serikali  ilikuwa sh.Miln 470 hata hivyo Halmashauri iliongeza sh. Miln 70 kutokana na kupanda kwa gharama za ujenzi ili kukamilisha miundombinu yote ya Shule hiyo itakayokuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita

Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Edward Jidamva ameeleza kuwa shule hiyo tayari imesajiliwa na wanafunzi 230 waliokuwa wakitembea zaidi ya kilomota 15 kuifuata shule ya Sekondari Miembesaba watakiwa wanufaikaji wa mwanzo

Diwani wa Kata ya Viziwaziwa Mohamedi Chamba amesema kitendo cha Serikali ya awamu ya sita kujenga shule hiyo ni mwendelezo wake wa kuitekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 kuhakikisha kila kata inapata shule ya Sekondari.

No comments: