Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa akizungumza KATIKA hafla ya utiaji saini mikataba nane ya ujenzi WA majengo Utalii na viwanja vya ndege |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas akizungumza KATIKA hafla hiyo |
Na: Pamela Mollel,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa hakutakuwepo na muda wa nyongeza katika utekelezaji wa miradi nane ya REGROW yenye thamani ya sh, bilioni 157.2.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba nane ya ujenzi wa majengo ya utalii,ujenzi wa viwanja vya ndege aliisisitiza hatasita kuwachukuliwa hatua wakandarasi watakao zembea kumaliza kazi kwa wakati sahihi kwa kuwa miradi hiyo imechelewa sana kufanyikana kwa zaidi ya miaka minne sasa
Alisema viwanja sita vya ndege vitajegwa ikiwemo Hifadhi za Ruaha viwanja vitatu, Hifadhi ya Mwalimu Nyerere viwanja viwili na Hifadhi ya Mikumi kiwanja kimoja
Waziri aliongeza kuwa katika hifadhi ya Udzungwa itajengwa njia njia ya juu ya utalii ya kilomita moja ambayo itakuwa njia ndefu katika njia zote Kusini mwa Afrika au Katika Nchi zaAfrika Mashariki.
Alitoa rai kwa wakazi wa mikoa ya kusini kuchangamkia fursa hivyo ya ujenzi wa miradi hiyo ili waweze kujipatia kipato
Aidha aliwataka Shirika la hifadhi za Taifa Tanapa kukuza utalii Kusini mwa Tanzania ili watanzania waone thamani ya miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini
"Acheni ukiritimba lazima tubadilike miradi huu u
ulikuwa ufanyike mwaka 2019 mnapita huku mnaingia huku sasa hii si faida kwa nchi yetu, simamieni mikataba acheni ukiritimba katika utekelezaji wa miradi mbalimbali haiwezekani Rais Samia Hassan Suluhu aseme ameleta miradi Kusini halafu watu wanakwamisha hapa lazima tuhakikishe mambo yaliyokwama yanafanya kazi ndio maana tunakwamua mambo mbalimbali yaliyokwama "
Naye Katibu Mkuu waWizara hiyo,Dk, Hassan Abbas alisisitiza milango ya kufungua fursa za utalii Mikoa ya Kusini ifunguliwe ikiwemo kusaini mikataba hiyo nane kwaajili ya uboreshaji wa miundimbinu lengo ni kufungua fursa za utalii.
Alitoa onyo kali kwa maofisa manunuzi watakaokwamisha zoezi hilo kwa manufaa yao binafsi ili tu kukwamisha miradi hiyo kuwa atafute pa kwenda maana lengo la miradi ni kukamilika kwa wakati ili wafadhi ambao ni Benki ya dunia watoe mkopo mwingine
No comments:
Post a Comment