WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 13 WA TOA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 5 April 2023

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 13 WA TOA

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha tuzo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza KATIKA Mkutano WA TOA


Na Mwandishi wetu Dodoma


maipacarusha20@gmail.com


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Aprili 4, 2023 amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa 13 wa TOA (Tanzania Local Government Reforms Association) kwenye ukumbi wa Jiji, Mtumba, jijini Dodoma.


akizungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Majaliwa amewataka viongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Umoja wa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri unaohusika na maboresho ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) wahakikishe kunakuwa na ushirikishwaji wa karibu wa wananchi katika kuainisha changamoto zinazowakabili na kuwawezesha kupanga na kutekeleza afua za kukabiliana na changamoto hizo kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka.

 


Pia ameitaka Ofisi ya Rais (TAMISEMI) ihakikishe Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka inakamilika mara moja ili iwezeshe taasisi zote nchini kupata mwongozo wa namna ya kutekeleza dhana hii muhimu kwa utoaji wa huduma na maendeleo ya wananchi.

 

“Kwa nafasi zenu, wekeni mikakati ya ukusanyaji na udhibiti wa mapato ya ndani ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.  Hii iwe sambamba na kubuni vyanzo vipya vya mapato, kufanya mapitio ya viwango vya ushuru na kuwa na takwimu sahihi za walipa kodi,” amesisitiza.

 


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TOA, Bw. Albert Msovela ambaye pia ni RAS wa Kigoma alisema kupitia TOA wameweza kuongeza uwazi na uwajibikaji katika ngazi ya msingi, utekelezaji wa LRGP I & II na matumizi ya Mfumo wa Fursa na Vikwazo ulioboreshwa (yaani improved O&OD).

No comments: