AFUNGWA MIAKA 30 BAADA YA KUBAKA MWANAFUNZI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 11 May 2023

AFUNGWA MIAKA 30 BAADA YA KUBAKA MWANAFUNZI




 NA : JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA 


maipacarusha20@gmail.com 


MAHAKAMA ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemuhukumu Mangode Rajabu (23),Mkazi wa Soga Wilaya ya Kibaha kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi .


Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 4/ 2023 imetolewa Mei 10, 2023 na Hakimu Fahamu Kibona wa mahakama ya Wilaya ya Kibaha wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.


Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Fahamu Kibona alieleza kuwa amejiridhisha kumtia hatiani mshitakiwa huyo kwa Mujibu wa kifungu 130 (1), (2) (a) na kifungu 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.


Imedaiwa Mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Novemba 7, 2021 huko Soga,Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment