Dkt. GWAJIMA APONGEZA MKOA WA ARUSHA KWA KUWA NA MKAKATI BORA WA KUSHUGHULIKIA KESI ZA UKATILI WA JINSIA NA WATOTO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 4 May 2023

Dkt. GWAJIMA APONGEZA MKOA WA ARUSHA KWA KUWA NA MKAKATI BORA WA KUSHUGHULIKIA KESI ZA UKATILI WA JINSIA NA WATOTO

 





Na Mwandishi wetu, ARUSHA

maipacarusha20@gmail.com


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa Pongezi kwa Mkoa wa Arusha kwa mikakati mizuri ya kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia na watoto.


Waziri Dkt. Gwajima ametoa pongezi hizo  alipotembelea Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Arusha na Dawati la Jinsia Polisi Mkoa wa Arusha Mei 04, 2023 kwa lengo la kupata uelewa kuhusu ushirikiano wa taasisi hizo katika kushughulikka kesi za ukatili wa kijinsia na watoto. 


Akiwa kwenye taasisi hizo Waziri Dkt. Gwajima amesisitiza umuhimu wa mamlaka zote kuanzia Maafisa Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka na Polisi kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha wananchi hasa wa chini wanapata haki.






No comments: