MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA SERIKALI DHIDI YA WANANCHI WA LOLIONDO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 15 May 2023

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA SERIKALI DHIDI YA WANANCHI WA LOLIONDO

 



Mwandishi wetu, Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Mahakama kuu Kanda ya Arusha,leo imetupilia mbali pingamizi la serikali katika kesi ya wananchi watano wa tarafa ya loliondo ,wilaya ya Ngorongoro ambao wanapinga zuia la wananchi kuingiza mifugo Katika pori tengefu la Pololeti.


Wananchi hao, wanaiomba mahakama kuitaka Serikali kuondoa zuio  hilo la kuingia kwenye eneo lenye kilomita za mraba 150O  ambalo wamekuwa wakitumia kwa ajii ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya kufanyia shughuli za imani yao 


Wananchi hao pia wanaiomba Mahakama itengue Tangazo la Serikali   la tarehe 17 Juni 2022  kuanzishwa pori hilo kwani ni batili na limetangazwa kinyume na sheria na pia haikuwashirikisha wananchi kama sheria inavyotaka


Lakini pia wanaomba  Mahakama itamke kuzuia Serikali na Mawakala wake wasifanye oparesheni zote kwenye eneo hilo.


Hata hivyo,kabla ya kuanza kusikilizwa shauri hilo,namba 21 ya Mwaka 2022 kuhusu maombi ya mapitio ya Sheria (Judicial Review Application) dhidi ya Tangazo la Waziri wa Mali asili na Utalii (GN no 421 ya tarehe 17 Juni 2022 kuhusu ardhi hiyo, serikali iliweka pingamizi.


 Jaji Joachim Tiganga alisema pingamizi la serikali kuwa watuma waombi walichelewa kuwapa maelezo ya maombi yao lilipaswa kwenda mbele zaidi kueleza litaathiri vipi kuendelea kwa kesi hiyo.


Jaji alisema mahakama imepanga kusikiliza shauri hilo Mei 29, saa sita mchana.


Hata hivyo,upande wa Jamuhuri  haukuwepo mahakamani wakati shauri hilo likitolewa maamuzi madogo na wananchi hao wa Loliondo walikuwa wanawakilishwa na Wakili Denis Moses.



No comments: