NDOA YA INSPEKTA BABU YAWAVUTIA WAKAZI WA ARUSHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 21 May 2023

NDOA YA INSPEKTA BABU YAWAVUTIA WAKAZI WA ARUSHA

 





Na Pamela Mollel,ARUSHA

maipacarusha20@gmail.com

MKAGUZI wa Jeshi la Polisi,Ally Babu amefunga ndoa ya kijeshi na mchumba wake,Selani Sumai na tukio hilo, lilikuwa kivutio kwa watu walioshiriki kutokana na kufanyika kwa matukio mbalimbali ya kijeshi ikiwamo kupigwa kwa gwaride la nguvu wakati wa sherehe hiyo.


Ndoa hiyo ya kijeshi ilifungwa mwishoni mwa wiki jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na viongozi wa Serikali.


"Kwa kweli imekuwa siku muhimu katika maisha yangu kwa kufanya jambo la kipekee ambalo linafungua njia na taswira nyingine kwa sisi wawili,"alisema Babu


Alisema kama ilivyokuwa kwa binadamu wengine Mungu amependa wawili hao kuwa kitu kimoja na kwenda kuanzisha mchakato wa maisha mapya ambayo yatakuwa sehemu kuunda familia bora na imara itakayokuwa ya mfano katika Jamii.


"Tuna mshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli yetu ya ndoa hii kufungwa nina furaha na tunatarajia kuishi maisha ya furaha na upepo ambayo yatakuwa mfano kwa wengine kuiga,"alisema Sumai



No comments: