RUFAA KESI YA UTOZAJI FAINI LAKI MOJA KWA NG'OMBE HIFADHINI YAAHIRISHWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 29 June 2023

RUFAA KESI YA UTOZAJI FAINI LAKI MOJA KWA NG'OMBE HIFADHINI YAAHIRISHWA

 


Na: Mwandishi wetu ARUSHA


maipacarusha20@gmail.com


Maamuzi ya  Rufaa ya kesi ya Jinai Namba. 9 ya 2023 inayopinga utozaji wa shilingi 100,000 kwa ng’ombe iliyotarajiwa kutolewa uamuzi  mbele ya Jaji Gwae imeahirishwa mpaka tarehe 28 Julai 2023 baada ya walalamikiwa kuarifiwa kwamba Jaji anayehusika na kesi kutokuwepo mahakamani hapo.


Katika rufaa hiyo inayowahusisha waomba rufaa wawili wakazi wa Ngorongoro wanaomba Mosi utozaji wa faini ya shilingi 100,000 kwa kichwa cha ng’ombe wanaokamatwa hifadhini ni batili na ni kinyume cha sheria.


Pili Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) haina mamlaka ya kutoza faini kwenye sehemu ambazo zimeanzishwa na Sheria ya Wanyama Pori, Sura 283 ambayo mwenye mamlaka ni mkurugenzi wa wanyamapori.


Aidha waomba rufani hao wanaainisha pia Kutoza faini ya shilingi 25,000 kwa kondoo ni batili na ni kinyume cha sheria.


Pia Kutoza faini ya 13,000,000 ni kinyume cha kiwango kilichowekwa na sheria.


Walalamikiwa KATIKA kesi hiyo ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ,Mkurugenzi wa wanyamapori na Jamhuri.

No comments: