UHABA MKUBWA WA MADAKTARI WA AFYA YA MIFUGO NCHINI. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 26 June 2023

UHABA MKUBWA WA MADAKTARI WA AFYA YA MIFUGO NCHINI.

 

Afisa Rasilimali watu na Mnyororo wa thamani wa Mifugo wa Shirika la chakula na Kilimo Dunia (FAO) Dr Moses Ole Nesellea akitoa mada

Afisa Rasilimali watu na Mnyororo wa thamani wa Mifugo wa Shirika la chakula na Kilimo Dunia (FAO) Dr Moses Ole Nesellea akitoa mada


Mwandishi wetu, Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Kuna uhaba mkubwa wa Madaktari wa Afya ya Mifugo nchini hatua ambayo inachangia sekta ya Mifugo kushindwa kutosheleza Soko la ndani na nje.


Akizungumza na waandishi wa habari Leo baada ya kufungua mkutano wa wadau wa sekta ya Mifugo kuhusiana na changamoto ya Madaktari wa Mifugo, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Profesa Hezron Nonga, amesema mikoa yenye Madaktari wa Mifugo ni 12 tu.


Amesema Kati ya halmashauri 184 Halmashauri 80 hazina  Madaktari wa Afya ya Mifugo.




Profesa Nonga amesema, kutokana na uhaba wa watumishi hao, kumekuwepo na ongezeko la magonjwa ya Mifugo ikiwepo magonjwa yanayosambazwa na Mbung'o , Kupe na Ugonjwa wa Kimeta .


Akitoa mada katika mkutano huo Afisa Rasilimali watu na Mnyororo wa thamani kwenye Mifugo wa Shirika la Umoja WA mataifa la chakula na Kilimo(FAO), Dk Moses Ole Neselle amesema  Shirika hilo limedhamini mkutano huo wa wataalam wa Mifugo ili kutatua changamoto za sekta ya Mifugo hasa uhaba wa watumishi.


Amesema ni vigumu sekta ya Mifugo kukuwa kwa kasi kama hakuna wataalam wa kutosha hadi ngazi za Kata ambapo ndipo kuna wafugaji 


Amesema kama yanahitajika matokeo makubwa katika sekta  ya Mifugo ni muhimu kuwekeza katika kuwepo wataalam wa kutosha.


Amesema hivi sasa kuna ongezeko la magonjwa ya Mifugo hivyo ni muhimu kuwepo wataalam wa kutosha.


Hata hivyo, amesema kupitia taarifa ya mshauri elekeze Wamoja Ayoub ambayo itawasilishwa katika mkutano huo inatarajiwa mapendekezo yake kusaidia kukuza sekta ya Mifugo.


Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Profesa Hezron Nonga


No comments: