WATALII WAONGEZEKA NCHINI KUTOKANA NA UTANGAZAJI VIVUTIO VYA UTALII, Mtoto wa Trump atembelea Ziwa Natron, avutiwa na uwindaji wa Kitalii - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 7 June 2023

WATALII WAONGEZEKA NCHINI KUTOKANA NA UTANGAZAJI VIVUTIO VYA UTALII, Mtoto wa Trump atembelea Ziwa Natron, avutiwa na uwindaji wa Kitalii







Mwandishi wetu, longido

maipacarusha20@gmail.com


Mtoto mkubwa wa kiume wa Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump, Donald Trump Junior, ambaye ni bilionea anayesimamia makampuni ya Baba yake amefika nchini kutalii.


 Trump junior anaendelea kutalii katika eneo la pori la Ziwa Natron kaskazini ambapo ni kitalu Cha uwindaji wa kitalii.


Trump leo  amefanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa na kuelezwa fursa za utalii zilizopo nchini huku akifurahia kuwepo nchini kutalii.

Trump Junior ni wa Rais Mwandamizi katika kampuni kubwa ya baba yake ya Trump Organization, akitajwa kuwa na utajiri unaofikia shilingi bilioni 750.

Trump  ameahidi kutembelea maeneo mbalimbali zaidi ikiwemo eneo la Mamlaka ya hifadhi ya  Ngorongoro na hifadhi nyingine


Waziri Mchengerwa  akizungumza na Trump amemuomba  kuwa balozi Utalii wa Tanzania kwani ina vivutio vingi vya Utalii .


Waziri Mchengerwa alimweleza mgeni huyo mashuhuri mwelekeo wa sekta ya utalii na fursa mbalimbali za uwekezaji. 

Amesema ujio wa Trump ni mafanikio ya filamu ya Royal Tour ambayo iliongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema ujio wa wageni maarufu ni faraja kubwa katika ukuaji wa utalii hapa nchini.





No comments: