WAZAZI KARATU WATAKIWA KUKAA KARIBU NA WATOTO WAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 3 June 2023

WAZAZI KARATU WATAKIWA KUKAA KARIBU NA WATOTO WAO

 



Na: Sofia Fundi, Karatu

maipacarusha20@gmail.com

Wazazi na Walezi wilayani KARATU mkoani Arusha wametakiwa  kukaa karibu na watoto wao katika kipindi hichi Cha likizo ili kupunguza vitendo vya kikatili dhidi yao.


Kauli hiyo imetolewa na Afisa maendeleo ya jamii bi Adelaida Shauri wakati akizungumza na baadhi ya wenyeviti wa vitongoji waliokuwa katika kikao Chao katika ukumbi wa halmashauri.


Bi Adelaida amesema kuwa matukio mengi hutokea hasa wakati watoto wakiwa likizo hivyo aliwaomba wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili.


"Wazazi na Walezi tuache kuwaachia watoto wawe huru masaa yote tuwape kazi za kufanya ili wasipate muda wa kuzurura na kufanyiwa vitendo vya kikatili"amesema Adelaida.


Amesema matukio  ya ukatili yamezidi  katika jamii  na baadhi husababishwa na wazazi kwa kuwaamini wanaowaachia watoto wao  hivyo aliwaomba kuacha Tabia ya kuwaamini ndugu.


Aliwaomba wenyeviti wa vitongoji kutoa elimu kwa jamii kujua wajibu wao wa malezi ya mtoto na kutoa matukio ya ukatili dhidi yao wanayofanyiwa katika maeneo yao.


"Jamii tunaomba ukimwona mtoto yuko sehemu isiyosahihi msemeshe na umwondoe hata kama siyo wa kwako kwani kipindi hichi Cha likizo watoto watakuwa wakizurura hovyo mtaani"alisema Adeleida.

No comments: