![]() |
| Dkt. Tulia Ackson akipongezwa baada ya kuchaguliwa |
Na: Mwandishi wetu Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson, kapitishwa na Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC),kugombea nafasi ya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU).
Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Octobar 27, mwaka huu nchini Angola.
Mbunge wa bunge la Afrika ya Kusini,Darren Bergman ndiye aliwasilisha hoja katika bunge hilo ,katika kikao cha 53 cha Jukwaa la Mabunge ya SADC kinachoendelea jijini Arusha na kuomba Mabunge yote kumuunga mkono Dk Tulia.
Amesema ametoa hoja ya kupitishwa Dk Tulia kuwania nafasi hiyo, kwa mujibu wa kanuni ya 26(4) ya utaratibu katika bunge hilo.
Amesema amewasilisha hoja ya kupata mgombea mmoja kutoka SADC, licha ya kuwepo wagombea wengine walioonesha nia kugombea nafasi hiyo kutoka Afrika.
Wagombea hao ni Catherine Gotan Hara wa nchini Malawi na Jacob Fransis Nzwidamilimo Mudenda wa Zimbabwe na Adji Diarra Megane Kanoutee wa mbunge kutoka Senegal.
Bergman amesema ili kuonesha Umoja katika kuwania nafasi hiyo,ni vyema kumpitisha Dk Tulia Spika wa Bunge la Tanzania, kutokana na sifa alizonazo kuwa mgombea wa SADC katika uchaguzi huo.
Hoja ya Mbunge huyo wa Afrika Kusini, iliungwa mkono na Mbunge kutoka nchini, Angola Pedro Sebastiano na kueleza kwa kuwa kwa muda mrefu nafasi hiyo, imekuwa ikishikwa na wabunge wanaume kumpitisha Dk Tulia ambaye ni msomi na kijana kuwania nafasi hiyo ushindi utapatikana.
"Naunga mkono hoja hii na ninawaomba wabunge wenzangu tuunge mkono,ili kuonesha umoja na mshikano ndani ya SADC hasa kuwa na mgombea mwanamke na ni kijana"amesema
Akizungumza baada ya kutolewa hoja hiyo, Rais wa Bunge la SADC,Roger Mancienne alitoa fursa ya wabunge kuchangia hoja hiyo, ambapo wabunge kutoka nchi za Zimbabwe, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lesotho,Zambia,Eswatini Namibia, Afrika Kusini, Mauritania walieleza kumuunga mkono Dk Tulia.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchaguliwa kuwania nafasi hiyo, Dk Tulia aliwapongeza wabunge wote kwa kumpitisha na kuwania nafasi hiyo ya kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani.
Amesema heshma aliyopewa ni kubwa kwani kuteuliwa kugombea nafasi hiyo katika bunge hilo lililoanzishwa tangu mwaka 1889 hadi sasa likiwa na wawakilishi wa mabunge 179 duniani.
Dk Tulia tayari amepitishwa pia na Bunge la Afrika(PAP) na Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EALA) kuwania nafasi hiyo.


No comments:
Post a Comment