![]() |
| RAIS WA awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na vijana WA jamii ya wahadzabe walipotembelea jamii hizo hivi karibuni |
![]() |
| Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na wamama WA kihadzabe walipitembea jamii hizo hivi karibuni |
Na Mwandishi wetu KARATU
maipacarusha20@gmail.com
RAIS WA awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wametembelea jamii ya Wahadzabe na kujifunza Mila na desturi zao za asili za kutafuta na kuhifadhi vyakula, malezi ya watoto na makazi yao.
Pia walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ya mila za jamii hiyo inayoishi katika zama za kale za kula matunda na asali.
Pamoja na mambo mengine waliweza pia kuongea kwa kina na jamii hiyo kuhusu changamoto zinazowakabili kama upatikanaji wa elimu kutokana na mfumo wao wa maisha wa kuhamahama, uvamizi wa makabila mengine katila maeneo yao ya asili hali inayotishia mtindo wao wa maisha pamoja na upatikanaji wa huduma nyingine muhimu za kijamii.



No comments:
Post a Comment