![]() |
| Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Hawa Mwaifunga akichangia madam mapema leo |
![]() |
| Rais Bunge la SADC akiingia bungeni |
Mwandishi wetu,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Hawa Mwaifunga amezitaka nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo kutekeleza Mkataba wa Malabo wa kutenga asilimia 10 ya fedha katika bajeti Kuu za serikali.
Mwaifunga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula, Kilimo na Maliasili,akitoa maelezo kuhusu hoja iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ishmael Onani kupitishwa kwa taarifa hiyo alisema ni muhimu serikali kushirikiana na wabunge kutatua tatizo la uhaba wa chakula.
Mwaifunga alisema, wanawake wana mchango mkubwa katika kilimo katika ukanda huu, lakini wanakabiliwa na changamoto ambazo zinakwamisha uwezo wao kama wakulima.
Alisema tafiti zinaonyesha kuwa katika SADC, wanawake wanachangia zaidi ya asilimia 60 katika uzalishaji wa chakula na kutoa nguvu kazi kubwa zaidi katika sekta hiyo.
Mwaifunga amebainisha tafiti zinaonesha pia kilimo kimekuwa kikichangia ukatili dhidi ya wanawake wanaopitia viwango vya juu vya unyanyasaji kutoka kwa wasimamizi wa Kazi.
Katika Mkutano huo Bunge la Tanzania linawakilishwa na Wajumbe watano (5) wa Jukwaa hilo ambao ni Seleman Zedi, Shally Raymond, Hawa Mwaifunga, Dk. Alfred Kimea na Kassim Haji.
Awali.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Wabunge wa SADC ya Chakula, Kilimo na Maliasili (FANR) Onani akisoma taarifa ya Kamati hiyo katika kikao cha 53 cha Jukwaa la Mabunge wa SADC, alisema ni muhimu serikali katika nchi hizo kuchukuwa hatua za kukabiliana na upungufu huo wa chakula kwani watu million 41 katika nchi 10 za SADC wanakabiliwa na upungufu wa chakula
Onani alisema katika Utafiti uliofanyika katika nchi hizo, umebaini kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula imeshuka kutokana na changamoto ya ukame na mabadiliko ya Tabia nchi.
Mwenyekiti huyo alisema, ili kukabiliana na changamoto ya usalama wa chakula ni muhimu nchi iongeze fedha katika bajeti ya Kilimo kulingana na makubaliano ya Mkataba wa Malabo ambayo yanataka nchi kutenga asilimia 10 ya bajeti kwa ajili ya sekta ya Kilimo.
Alisema uhaba wa chakula pia umechangiwa na vita vinavyoendelea nchini Congo DRC lakini pia Vita dhidi ya Ukraine na Russian.
Onani alisema ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabia nchi ni vyema kuzuia matumizi ya kuni na Miata kutokana kuathiri misitu
"Lakini pia ni muhimu kuhimiza matumizi ya Nishati ya Gesi na Jua katika Jamii lakini pia kuwawezesha Vijana na Wanawake kushiriki katika kilimo"alisema
Alisema muhimu serikali katika nchi za SADC kushirikiana kukabiliana na upungufu wa chakula kwa kuongeza uzalishaji wa mazao,kijikita katika kilimo cha umwagiliaji na kusambaza pembejeo kwa wakati kwa wakulima.


No comments:
Post a Comment