![]() |
| Padre Pamphil Nada enzi za uhai wake |
NA: Mwandishi wetu, Karatu
maipacarusha20@gmail.com
Paroko wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Karatu Jimbo la Mbulu, Padre Pamphili Nada ameuwa kwa kupigwa na kitu kizito na kichaa aliyeingia Kanisani kwa nguvu kutaka kusali Misa za Asubuhi.
Hata hivyo baada ya kichaa huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30) kufanya mauwaji hayo nae akauawa na Wananchi wenye hasira.
Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho Cha Padre Leo Julai 19,2023 na pia kutokea mauwaji ya kichaa huyo.
"Padri alifariki wakati anapelekwa hospitali na Mtuhumiwa aliuwa na wananchi wenye hasira baada ya kupata taarifa za tukio hilo"amesema
Baadhi ya wakazi wa Karatu walisema Kichaa huyo, tangu usiku wa kuamkia leo alikuwa anataka kuingia Kanisani lakini walinzi walikuwa wanamzuia.
Muumini wa kanisa hilo Rehema Baha, alisema Asubuhi kichaa huyo akiendelea kupiga kelele kutaka kuingia kusali na ndipo Padri Nada alitoka nje na kumwambia mlinzi amfungulie mlango.
"Baada ya kichaa kuingia ndani akiwa na Padri tu Kanisani ndipo alichukuwa chuma Cha mlango na kumpiga Padri ambaye alifariki wakati akikimbizwa hospitali" amesema
Peter Yohana anasema kutokana na tukio hilo kengere ya Kanisa ilipigwa na wananchi kukusanyika na baada ya kupata taarifa hizo walianza kumpiga kicha na kusababisha kifo chake.
"Tunamfahamu huyu kichaa anatoka Kijiji Cha Gekum Rambo na amekuwa Karatu kwa muda Sasa" amesema Yohana.
Taarifa za pole zilizotolewa na Askofu wa Jimbo la Mbulu hizi hapa chini


No comments:
Post a Comment